Saturday 7 December 2013

Watoto wetu;Movie ya Leo-To Grandmother's House We Go,Burudani-Joe Mafela - Shebeleza

Pumzika kwa Amani Babu/Mzee MADIBA
Watoto wangu wapendwa natumaini hamjambo..Wazazi/Walezi Pia..
Natumaini wote tupo pamoja kwa Kuomboleza Kifo Cha Mpendwa wetu TATA MADIBA.

Niwakati mzuri sana kumuenzi kwa yote mema aliyotuachia.Amefanya mengi mengi sana..
Daima tutamkumbuka Mzee wetu MADIBA.

Leo tuangalie Movie hii,Twende sote sasa.......


Joe Mafela na Shebeleza....


Nawatakia kila lililojema,Baraka,Amani,Upendo,Umoja na Maandalizi mema ya Christmas.



Ni Mimi Mama/Shangazi yenu Rachel [Kachiki]
Nawapenda Wote.

Tuesday 3 December 2013

Kipindi cha familia kutoka Jamii Productuion...Majukumu ya Baba katika Familia


Karibu katika kipindi hiki cha FAMILIA kutoka Jamii Production.

Katika kipindi cha wiki hii, mjadala wa WAJIBU WA BABA KATIKA FAMILIA umefungua mfululizo wetu wa mijadala kuhusu wajibu wa mzazi kwa familia yake

Mbali na washiriki waliokuwemo studio, pia tumeshirikisha maoni toka kwa wasikilizaji wetu wapendwa waliyotoa kwenye ukurasa wa Facebook
Msimamizi wa kipindi Abou Shatry akifuatilia mjadala

Karibu uungane nasi



Mjadala ukiendelea
Mgeni wetu katika mjadala huu Isidory Lyamuya


--
*JAMII PRODUCTION*
"Usahihi wa fikra ndio fikra sahihi

Friday 29 November 2013

Watoto Wetu;Movie Ya Leo-An American Girl Chrissa Stands Strong (FULL MOVIE)

Nimatumaini yangu  Watoto wangu wazuri hamjambo,Wazazi/Walezi Pia.
Haya tuangalie hii movie ya Leo na inamafunzo sana.
Tuendeleeee......


Natumaini mmejifunza mengi.
Nawatakia siku njema.
Ni mimi Shangazi/Mama yenu Racchel[KACHIKI].

Wednesday 27 November 2013

Ukatili Kwa Watoto;Mtoto wa Miaka 5 Acharangwa Mapanga.


Mtoto mwenye umri wa miaka mitano, Benson Nilah (pichani), amejeruhiwa vibaya kwa kucharangwa mapanga akituhumiwa kuchuma mapera bustanini kwa mtu katika kijiji cha Madizini Manispaa ya Songea, mkoani Ruvuma. Mtoto huyo alijeruhiwa vibaya sehemu za usoni na mdomoni na kusababishwa ashonwe nyuzi sita, alipatwa na mkasa huo mwishoni mwa wiki iliyopita na anayetuhumiwa kufanya kitendo hicho ni Ronginus Haule (58), mkazi wa eneo hilo.
kusoma zaidi »http://www.chingaone.com/

Saturday 23 November 2013

Watoto Wetu;Hadithi Ya Leo-The Greatest Treasure Na Nyingine!!!!!!




Watoto Wangu Wazuri, Wazazi/Walezi nimatumaini yangu wazima kabisa na mnaendelea vyema .Poleni sana watoto wa Nga'mbo kwa Baridi..
Hadith ya Leo; The Greatest Treasure...Endeleeni....


Thanks;bookboxinc
Jee mmeipenda? Nini mmejifunza?

Basi tukutane wakati mwingine, Nawatakia kila la kheri,Baraka, Masomo Mema na Muwe watoto Wema,Wasikivu na kusaidia kazi za nyumbani.

Ni mimi Shangazi/Mama yenu;Rachel[KACHIKI].

Friday 15 November 2013

Watoto Wetu;Move Ya Leo-The Lion King,Burudani-USA for Africa - We Are The World ( Original Music Video 1985 )



Nimatumaini Yangu Watoto Wangu Wazuri,Wazazi/Walezi hamjambo na Mnaendelea Vyema.
Hapa tulipo Baridi imeshaanza..na Shamra Shamra za Christmas zimeshaanza....Vipi hapo mlipo?








Leo nimewaletea Move [sinema] The Lion King...



Burudani ;

USA for Africa - We Are The World ( Original Music Video 1985 )


Jee mmeipenda? na Nini mmejifunza?

Nawatakia Masomo mema,Maandalizi mema ya Christmas na Msisite kututumia picha.


Ni Mimi Mama/Shangazi yenu;Rachel [KACHIKI]

Monday 4 November 2013

TAMKO LA HAKIELIMU KUHUSU UPANGAJI WA VIWANGO VYA ALAMA, MATUMIZI YA ALAMA ENDELEVU YA MWANAFUNZI NA UFAULU 4 NOVEMBA 2013


 Hivi karibuni serikali imetoa tamko kuhusu mfumo mpya wa upangaji wa viwango vya alama, matumizi ya alama endelevu ya mwanafunzi na ufaulu. HakiElimu na wadau wake imetafakari tamko hilo na kutoa maoni ya yafuatayo:

 1. Hatujatambua lengo la serikali kuleta mabadiliko haya; hasa ikikumbukwa kuwa Tume ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, Mh. Mizengo Pinda haijawahi kuweka bayana taarifa yake kuhusu sababu za wanafunzi kutofaulu vizuri katika mitihani ya kumaliza kidato cha nne. Wajumbe wa Tume hiyo wamekuwa wakitoa dondoo fupi fupi za matokeo ya kazi yao-kama vile Bungeni na katika hadhira nyingine za kitaifa; bila kutoa ripoti yenyewe. Je, kwa mabadiliko haya,wizara inataka kuwaaminisha Watanzania kwamba alama zilivyokuwa zimepangiliwa hapo awali,ndiyo sababu kuu ya wanafunzi kutofaulu vizuri? 

 2. Wizara imeeleza kwenye tamko lake kwamba imeshirikisha wadau mbalimbali katika kufikia uamuzi huo. Hata hivyo, katika orodha ya wadau walioshirikishwa inaonekana bayana kuwa asasi za utetezi hazikupewa nafasi. Baada ya kufanya mawasiliano na baadhi ya wadau wanaodaiwa kushiriki,wenyewe wamekiri kuwa ingawa walishiriki mawazo yao hayakuzingatiwa na hawakukubaliana kuhusu kushusha alama za ufaulu kufikia 20 kati ya 100.

 3. Mpangilio wa alama zitakazotumika kuanzia mwaka huu unaleta tafsiri ya ndani kuhusu nia ya wizara kubadilisha alama hizo. Tafsiri hiyo ni kulazimisha kuona kwamba wanafunzi wachache zaidi wanapata daraja la 5 (ambalo limeanzishwa badala ya daraja sifuri); kukiwa na uwezekano wa kupunguza wanafunzi wanaopata daraja hili kwa asilimia 2.2% ukilinganisha na utaratibu uliotumika kwa matokeo ya mwaka 2012. Mpangilio huo mpya una uwezekano wa kuongeza kundi la wanafunzi wanaopata daraja la tatu na la nne kwa asilimia 12.1% kuliko utaratibu uliotumika mwaka 2012. Hata hivyo, alama hizo mpya zinaweza kupunguza uwezekano wa kupata daraja la kwanza na la pili kwa asilimia 11.9%. Serikali na wadau wengine wa elimu wanatambua bayana kuwa njia kuu ya kuboresha elimu na matokeo katika mitihani ni kuboresha utaratibu wa utoaji wa elimu. Kwa nini serikali, hasa katika kipindi hiki inataka kuona matokeo mazuri bila kuwekeza kwenye mipango ya kuboresha mfumo na utaratibu wa utoaji wa elimu? HakiElimu inatafsiri uamuzi huo wa serikali kama ni kukwepa ukweli na utaalamu; na badala yake serikali inatafuta njia ya mkato ya kuwafurahisha wazazi na wananchi ili wapunguze kelele.

 4. Serikali imekubali kutumia asilimia 40 kutoka kwenye Alama za Tathmini Endelevu ya Mwanafunzi (Continuous Assessment, CA), ili ziunganishwe na alama 60 za mtihani wa mwisho. Hata hivyo, uzoefu unaonesha kuwa alama hizo zilikuwa zinachakachuliwa huko shuleni, na hata Baraza la Mitihani Tanzania mwaka huu walikiri hilo kutokea. Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi itatumia njia gani kuhakikisha kuwa zinapatikana alama sahihi toka shuleni zinazoendana na uwezo wa mwanafunzi? Je, kwa kiasi gani walimu wameandaliwa na kujengewa mazingira mazuri ya kufanikisha zoezi hili? Hata hivyo, serikali inapaswa pia kuwaeleza watanzania uzoefu wa nchi nyingine za Afrika katika matumizi ya alama za CA; wengine wanatumia asilimia ngapi? Ni muhimu kuwa na ushahidi kuwa kiwango cha CA tutakachokitumia kitaboresha utaratibu wa kutathmini wanafunzi; na kuwatendea haki badala ya kuwaghiribu au kuwaumiza. 

 5. HakiElimu inasikitika kuona wizara inalazimisha kila mwanafunzi atakayefanya mtihani wa kidato cha nne au cha sita awe amefaulu. Hiyo inathibitishwa na tafsiri ya alama ambazo zitatumika zinazoonesha kwamba kuanzia atakayepata alama sifuri mpaka mia moja atakuwa amefaulu kwa namna fulani. Kwa mfano, hata atakayepata alama kuanzia 0 mpaka 19 katika somo fulani atahesabiwa kuwa amefaulu, japo katika kiwango kisichoridhisha. Kwa nini wizara inakosa ujasiri wa kukubali kuwa mwanafunzi atakayepata chini ya alama fulani ahesabiwe kuwa hakufaulu? 

 6. Kwa upangaji huo mpya wa alama za ufaulu, Tanzania itakuwa nchi ya kwanza katika bara la Afrika kwa kuwa na kiwango cha chini kabisa cha ufaulu katika elimu ya sekondari na kuna hatari kwamba kushushwa kwa alama za ufaulu kutapunguza ama kuondoa hamasa ya wanafunzi kusoma kwa bidii, kwa kuamini kuwa hawatafeli na cheti watapata tu. Kama wadau wote tunakubaliana kuwa nia ya kutoa elimu ni kuandaa Watanzania ambao watakuwa na maarifa na uwezo wa kushindana na wengine wanaosoma katika nchi nyingine Afrika. 

 7. HakiElimu pia inasikitika kuona kuwa wizara inapotosha malengo ya “Matokeo Makubwa Sasa (Big Results Now-BRN)” kwa kutafuta njia za mkato. BRN imeeleza bayana kuwa kati ya mikakati itakayotumika kupata Matokeo Makubwa katika elimu ni kuboresha mchakato wa kufundisha na kujifunza shuleni na kuboresha utaratibu wa utoaji wa elimu kwa kuweka bayana majukumu ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi na ile ya TAMISEMI. Wizara iwaambie Watanzania kuwa kwa kiasi gani upangaji huu wa alama utasaidia kuboresha mazingira ya ufundishaji na ujifunzaji kwa maana ya kumjengengea mwalimu uwezo, mazingira mazuri na hamasa ya kufundisha na pia kutengeneza mazingira mazuri ya mwanafunzi kujifunza. Katika haya, je, ni kweli kwamba huu upangaji upya wa madaraja ni kipaumbele chetu namba moja? Si busara kushughulikia mpangilio wa alama na madaraja kwanza wakati mchakato wa kuboresha mfumo wa elimu ili kupata hayo matokeo mazuri bado uko chini. Kitendo hicho ni kukurupuka na kuruka hatua muhimu zinazoweza kuboresha elimu.

 8. HakiElimu inawatahadharisha Watanzania, wakiwemo wazazi, wanafunzi na vijana wenye nia ya kurudia mitihani ili wapate vyeti; na serikali yenyewe kuzingatia ukweli kwamba: Elimu ni uwezo, SIYO cheti. Jitihada za Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi zinaonesha wazi kuwa nia ni kuona matokeo mazuri hata kama matokeo hayo hayataendana na uwezo walio nao wanafunzi. Katika kutengeneza raslimali watu ya kutosha, Tanzania kama ilivyo kwa nchi nyingine haina namna ya kukwepa kuhakikisha kwamba mfumo wa elimu unaandaa vijana au wananchi wenye uwezo wa kukabiliana na changamoto zinazowakabili wao wenyewe, jamii na Taifa kwa ujumla; pia kuwa na wananchi ambao watakuwa na ujasiri, tija na ubunifu, katika uzalishaji katika shughuli na fursa mbalimbali watakazozipata au kuzitafuta. Hali hii haipatikani kwa kuhangaika na alama za ufaulu kama kipaumbele. Tunahitaji kuhangaika na mfumo wa utoaji elimu utakaotusaidia kuleta mapinduzi ya kweli ya kiuchumi, kijamii na kisiasa. HakiElimu inaishauri Serikali kusitisha matumizi ya alama na madaraja haya mapya. Irudi kwa wadau na ushahidi kuhusu uamuzi huu; huku ikitoa nafasi ya kuchukua maoni ambayo yanaweza kuboresha mfumo wa upimaji wa wanafunzi. Wakati zoezi hilo linaendelea, HakiElimu inaisisitiza Serikali kutumia matokeo ya tafiti mbalimbali na mipango iliyopo kushughulikia dosari na changamoto zinazorudisha nyuma elimu yetu, hasa zile zinazokwamisha ufundishaji na ujifunzaji shuleni. Tamko hili limesainiwa na,
 Elizabeth Missokia Mkurugenzi Mtendaji, HakiElimu.

Kipindi cha FAMILIA kutoka Jamii Production......FAMILIA ZA KAMBO (sehemu ya mwisho)‏



Mtayarishaji na mtangazaji wa kipindi cha FAMILIA, Georgina Lema
Moja ya sababu zilizotusukuma kujadili masuala kuhusu FAMILIA ZA KAMBO ni takwimu zilizopo hivi sasa kuhusu familia hizi.
Kwa mujibu wa mtandao wa www.blendedandbonded.com, hapa Marekani
• 41% ya ndoa za kwanza huishia kwenye talaka
• 60% ya ndoa za pili huishia kwenye talaka
• 73% ya ndoa za tatu huishia kwenye talaka
• 45% ya wanawake na 50% ya wanaume wataoa tena ndani ya miaka mitano ijayo
• 50% ya ndoa za marudio huhusisha watoto wa mahusiano yaliyopita walio chini ya miaka 18
•Ndoa 2100 huanzishwa kila siku nchini Marekani
• 42% ya watu wazima wana uhusiano wa kambo. Hii inajumuisha mzazi wa kambo / mtoto wa kambo ama ndugu wa kambo
Kwa idadi ya Marekani, takwimu hizi zinamaanisha kuwa familia za kufikia zinahusisha watu wazima wapatao milioni 95.5
•Kuna baba wa kambo milioni 16.5
•Kuna Mama wa kambo milioni 14.
•Wataalamu wa mahusiano wanasema kuwa ndoa za kufikia ndio zitakuwa ndoa zenye umaarufu na nyingi zaidi nchini Marekani na kuwa, kutokana na kukosekana kwa taarifa sahihi kuhusu familia za kufikia, familia hizi mara nyingi zimejikuta kwenye migogoro na mafarakano.
Nasi tuko hapa kujaribu kuepusha hilo kwa kushirikiana nanyi katika kile tunachoweza kuelimisha kudumisha ndoa hizo.
Ungana nasi katika sehemu hii ya mwisho ya MADA hii.
-- *JAMII PRODUCTION* "Usahihi wa fikra ndio fikra sahihi"

Friday 1 November 2013

Watoto Wetu Move Ya Leo;It Takes Two..!!!

Nimatumaini yangu Watoto wangu Wazuri mnaendelea vyema.Wazai/Walezi pia.
Maandalizi ya Christmas hapa tulipo yamesha anza..Vipi hapo ulipo wewe?
Move[sinema] ya Leo,It Takes Two... haya tuendelee kuangalia.


Jee mmejifunza nini kupitia Move[sinema] ya Leo?
Nawatakia kila la kheri,mpendane,Msaidiane na Mshirikiane vyema.


Ni Mimi;Shangazi/mama yenu Rachel[KACHIKI]

Saturday 26 October 2013

Watoto Wetu Hadithi Ya Leo;Sungura na Mama mwenye shamba,Burudani- Kutoka kwa Mrisho Mpoto,Kwani ni Yeye MAMA!!

Watoto kipindi cha Baridi Kimeanza hapa tulipo.




Ni matumaini Yangu Watoto.Wazazi/Walezi Mnaendelea vyema kabisa na majukumu yenu..
Hapa tulipo Baridi imeanza..Basi watoto msisahau kuvaa nguo nzito/makoti,masweta  kwa kujilinda/kujikinga na baridi...
Pia shule zimefungwa kwa Wiki Moja..Basi Watoto Wangu wapendwa Muda huu muutumie Vizuri na kujifunza meengi  katika Jamii yanayo wajenga zaidi.Pia Wazazi/Walezi wenzangu huu muda mzuri sana kwa kuwafundisha  watoto ya kwetu..Kama kazi ndogondogo kulingana na umri wao,Nidhamu,Heshima na mengine meengi.

Watoto wa Afrika na Nchi nyingine vipi huko kwenu?
Jee Hadithi ya Leo mmejifunza nini?


  Shukrani;http://hadithihadithi.podomatic.com


Ni Mimi;Mama/Shangazi Yenu,Rachel[Kachiki]

Wednesday 23 October 2013

Watoto Na Lishe Bora;da'Sophi Kajembe wa Tupike Pamoja..!!!!!


Pureed vegetables Mahitaji: Carrot 1 Boga (350 gr.) Kitunguu 1/2 Viazi 2 Chumvi Mafuta ya olive (3 Tbsp.) Ingredients: 1 Carrot Pumpkin (350 gr.) 1/2 Onion 2 Potatoes Salt Olive oil (3 Tbsp.)

This is a video showing how to cook a puréed vegetables (a special meal for children from 18 months to 4 years old), for East-African users and all the swahili speakers all around the world. It's also subtituled in English. Please, subscribe to our channel if you like it. We are working to offer you more video-recipes in swahili, in our Youtube channel and in our web-site www.tupikepamoja.com

Tuesday 15 October 2013

Mahojiano na wadau wa darasa la Kiswahili Washington DC‏

Photo Credits: Panafricanvisions.com
Kiswahili inaaminika kuwa lugha asili ya Afrika inayozungumzwa na watu wengi kusini mwa jangwa la sahara.
Kama tunavyojua, ni lugha ya taifa kwa nchi za Tanzania naKenya, na pia yazungumzwa kwenye nchi za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Burundi, Rwanda, Uganda na visiwa vya Comoro.
Ikizungumzwa na watu wanaokadiriwa kufikia milioni 100 hivi sasa, Kiswahili ndio lugha pekee ya kiAfrika iliyo miongoni mwa lugha rasmi za Umoja wa Afrika. Na inaaminika kuwa lugha ya saba kwa watumiaji wengi duniani
Na matumizi yake kama lugha inayozungumzwa na wengi wenye lugha tofauti katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati unaifanya lugha hii kuwa muhimu zaidi kwa watu wengi walio na mahusiano na / ama wanaotaka kujishughulisha na biashara, kazi ama diplomasia katika ukanda huo.
Kiswahili sasa kinafunzwa katika vyuo visivyopungua 50 hapa nchini Marekani, lakini pia inafundishwa kwenye vyuo vikuu mbalimbali Ulaya na hata bara Asia.
Kiswahili ni lugha muhimu katika habari, shule, kazi za kiofisi, kidiplomasia na hata usalama miongoni mwa mataifa na naamini ndio sababu hata jumuiya ya waTanzania hapa Washington DC wakaona ni jambo la busara kuanzisha darasa la kufunza Kiswahili kwa watoto hapa DMV.
Na leo, wawakilishi wa wahusika wa mpango huo, Rais wa Jumuiya ya waTanzania DMV (Washington DC, Maryland na Virginia) Idd Sandaly pamoja na walimu Asha Nyang'anyi na Bernadeta Kaiza wamekuwa wakarimu sana kujiunga nami katika studio za JAMII PRODUCTION hapa Washington DC.
KARIBU UUNGANE NASI
Rais wa Jumuiya ya waTanzania DMV (Washington DC, Maryland na Virginia) Iddi Sandaly akishiriki kipindi ndani ya studio za Jamii Production
Mmoja wa walimu wa darasa la Kiswahili hapa Washington DC Bernadeta Kaiza ndani ya studio za Jamii Production
Mmoja wa walimu wa darasa la Kiswahili hapa Washington DC Asha Nyang'anyi akishiriki kipindi ndani ya studio za Jamii Production
Twawapenda....Tukutane juma lijalo kwa kipindi kingine cha HUYU NA YULE tutakapohojiana na wadau wengine juu ya jambo jingine MUHIMU kwa jamii yetu
-- *JAMII PRODUCTION* "Usahihi wa fikra ndio fikra sahihi"

Saturday 12 October 2013

Watoto Wetu Katuni Ya Leo;Bongo Katuni-Kificho Animation!!!


Ni matumaini Yangu Watoto,Wazazi/Walezi wote Hamjambo na mnaendelea vyema.
Kwa  wale watoto wanaoishi Nga'mbo Mjiandae vyema na Baridi.
Na Wale Ndugu zetu Waislam tunawatakia Maandalizi mema ya Siku kuu  ya Eid.

Basi Nisiwachoshe,Leo nimewaletea Katuni[CARTOON].

Tuendelee....






Mmejifunza Nini Kupitia KATUNI[CARTOON]  Hii?
Shukrani;bongotoonz


Ni Mimi Mama/Shangazi Yenu Rachel [KACHIKI]

Dawati Ni Elimu Na Jerry Silaa!!!!


Jerry Silaa
Jerry Silaa;
 The "Dawati ni Elimu"” charity walk was be held on 12 October from Mnazi Mmoja to Bunge Primary School led by the first lady of United republic of Tanzania Mama Salma Kikwete. “The First of its kind mayoral ball aims to raise TZS 4.98 Billion towards providing 30,487 desks to primary and secondary schools in Ilala Municipality by end of financial year 2013/14. 100% of all funds shall proceeds towards realization of this project. Dawati Ni Elimu is a project by Hon Jerry Silaa, Mayor of Ilala Municipal council toward the build up of the annual Mayors ball. The Charity walk was sponsored by TSN Group, Eventlites, Continental Outdoor, A1outdoor and Vodacom and Managed by 361 degrees. ABOUT DAWATI Ni ELIMU. DAWATI Ni ELIMU is a project towards the Mayors ball that aims to solve the issue of shortage of desks in primary and secondary schools in Ilala municipality where by currently there is a lack of 30,487 desks. The project is an initiative under the office of the mayor of Ilala Municipal Council, this project seeks to raise a sum of 4.98 Billion Tanzanian shillings with the emphasis that the society can contribute and make change to solve the challenges by calling upon organisation and individuals to contribute to this noble cause.
See More;
 DAWATI NI ELIMU - charity walk 
Jerry Silaa;
;
DAWATI NI ELIMU;Kalisha mmoja Boresha Elimu!!!!!!

Wazazi/Walezi haya Tuungane Pamoja kusaidia watoto wetu wasikae Chini.

Shukrani;Jerry Silaa.

Saturday 5 October 2013

Watoto wetu ; Hadithi ya Leo-Nguruwe Watatu Wachanga!!!!




Natumaini Watoto,Wazazi/Walezi mnaendelea vyema.
Nini mmejifunza kupitia Hadithi hii?


Nawatakia Kila lililojema na mapumziko mema.

Shukrani;wambugu kamau

Ni Mimi Mama/Shangazi yenu;Rachel [KACHIKI]

Wednesday 2 October 2013

Watoto Na Maisha-Bethany Family children's home Tanzania!!!!!!

Wazazi/Walezi, Watoto..Leo "Watoto Na Maisha" Hawa ni Watoto wa Bethany Family Children's Home Tanzania...
Tukumbuke Leo tupo tuonaishi na Watoto wetu,Leo hii wapo wanaotamani kuishi na wazazi wao..Lakini kwa sababu zilizo nje ya uwezo wao hawawezi/haiwezekani.....

Wapo wengine wanatamani/kuhitaji kuishi kwenye Vituo hivi..lakini wanashindwa/hawajui vipi watafika hapa..bado wapo Mitaani,Kula,Kulala,Kuvaa ni shida.

Mmhhh.. siwezi kuelezea zaidi/Nisikuchoshe..Endelea Kuangalia Maisha ya Watoto hawa..
Wengi wao wanaonekana Wenye furaha  na Amani.. na MUNGU azidi kuwa siamami..


Mzazi/Mlezi nini umejifunza kupitia Video hii?
Nini Msaada wako kwa Watoto wenye shida/kuhitaji?
Nini unaweza kuwaambia Watoto wako?


kwa Maelezo Zaidi ingia;http://www.bethanyfamily.net/

Saturday 28 September 2013

Watoto Wetu Hadithi Ya Leo;Mbalamwezi Nyota Begani-Sehemu Ya 1-2.!!!!!!

Nimatumaini Yangu Watoto Wangu Wazuri Hamjambo na mnaendelea Vyema na Masomo pamoja na Maisha....
Wazazi/Walezi wenzangu pia natumani mko salama na mnaendelea na Utaufutaji wa mkate kwa watoto.


Mimi Mzima kabisa pamoja na Familia Yangu...Poleni sana nilipotea kidogo kwa sababu zilizo nje ya uwezo wangu..Nimepata email, sms/ ujumbe mbalimbali kutoka kwa baadhi ya wazazi/walezi na Watoto, Kujua mbona kimya? Asanteni Sana kwa kuwa nami na MUNGU azidi kuwa Nasi.

Watoto,Wazazi/Walezi wa "KENYA" Poleni Sana na yaliyotekea na MUNGU aendelee kuwapa Nguvu kwa Wakati huu Mgumu Kwenu.

Basi Nisiwachoshe;Leo nimewaletea Hadithi Ya Mbalamwezi Nyota Begani.Kutoka;
http://hadithihadithi.podomatic.com/[MAMA na MWANA]

Endelea kupata Raha.......




Hadithi ya Mbalamwezi Nyota Begani ni mojawapo ya Hadithi za Mama na Mwana toka Radio Tanzania. Kwa nakala ya hadithi hii na nyinginezo wasiliana na Radio Tanzania Dar es Salaam
Haya Watoto Nini Mmejifunza kupitia Hadithi Hii?
Wale Watoto ambao kiswahili kina wapa shida kidogo,Natumaini Wazazi/Walezi watawasaidia.
Niwatakie Mapumziko mema ya Mwisho wa wiki,Muwe watoto Wasikivu na Mzingatie Masomo.

Ni mimi Mama/Shangazi Yenu;Rachel siwa Isaac.
  Nawapenda Wote
.

Saturday 31 August 2013

Watoto Wetu;Hadithi ya Leo-Paka Wawili Wageuzwa Simba,Sehemu Ya-4-6!!!!!


Nimatumaini yangu Watoto Wangu Wazuri Hamjambo na Mnaendelea Vyema,Wengine mko kwenye maandalizi ya kurudi Shule,Wengine mmesharudi Shule.
Wazazi/Walezi nanyi nategemea mnaendelea vyema katika Malezi na Utafutaji.

Basi nisiwachoshe tuendelee na Hadithi yetu tuliyo ianza wiki iliyopita;Endela...







Jee mmejifunza nini kupitia Hadithi Hizi?
Nawatakia Mapumziko mema ya Mwisho wa Wiki.

Ni Mimi Shangazi/Mama Yenu Mpendwa;Rachel [KACHIKI]

Friday 23 August 2013

WatotoWetu;Hadithi ya Leo-Paka Wawili Wageuzwa Simba; Sehemu ya 1-3!!!!










Wazazi/Walezi na Watoto wangu Wazuri,Natumaini wote hamjambo na Mnaendele vyema na Masomo, Na wale waliokuwa kwenye Likizo ndiyo Inaishia sasa na Mnajiaanda kurudi Shuleni.

Hadithi  ya Leo,  Paka wawili wageuzwa simba ,
Shukrani;John Inniss

Mhhhhh Inatisha eehh..Haya Endelea kuangalia na itaendela...

Nawatakia mwisho mwema wa wiki,Na muwe watoto wasikivu na wenye kupendana.

Wenu;Shangazi/mama yenu;Rachel siwa[KACHIKI]

Asanteni Sana.


Saturday 17 August 2013

Watoto Wetu Leo;Hadithi ya Binti Chura,Sehemu Ya 1-2







Hadithi ya Binti Chura imepatikana toka katika Hadithi za Mama na Mwana Radio Tanzania. Kwa nakala ya hadithi hii na nyinginezo wasiliana na Radio Tanzania Dar es Salaam.
Tunaomba radhi kwa matatizo yoyote ya sauti katika hadithi hii


Watoto wazuri,Wazazi/Walezi, Nimatumaini yangu Mmefurahia sana Hadithi hizi...

Wazazi/Walezi/Watoto Wa zamani nini Maoni yenu katika vipindi vya sasa na vyazamani kwa Watoto?

Watoto;Nini mmejifunza kwenye Hadithi hizi?
Poleni watoto msiojua Kiswahili,Natumaini Wazazi/walezi watawasaidia Kuwatafsiria kwa Lugha mzijuazo.Pia natumai mtakuwa na hamu ya kujua Lugha hii ili msipitwe na Mambo mazuri/Kujifunza Meeengi ya Waswahili.

Niwatakie Mapumziko mema ya mwishoni mwa Wiki,Muwe Watoto wema na Watiifu kwa Wazazi/Walezi na Jamii pia.

Asanteni sana.
Shukrani;http://hadithihadithi.podomatic.com

Ni Mimi;Mama/Shangazi Yenu;Rachel siwa[KACHKI]

Friday 9 August 2013

Watoto Wetu Leo;Niwakumbushe Kipindi Cha MAMA na Mwana; Hadithi-siri ya Binti Mfalme;Sehemu ya 1-2.!!!!!!







Wapendwa watoto leo nawaletea Kipindi cha MAMA na Mwana. Wazazi/Walezi Leo nimewarudisha Nyuma/Zamani kidogo..Kuhusu MAMA na MWANA...Wengi wenu Mlikuwa/Tulikuwa wafuatiliaji wazuri sana..Enzi zetu na watangazaji wa RTD.Ninao wakumbuka..Shangzi/Mama;Sango Kipozi,Sarah Dumba,Debora Mwenda,Eda Sanga......Duhhh samahani kama nimekosea majina.
kulikuwa na Hadithi,Nyimbo,Vitendawili,Nyimbo,Kutembelea Mashuleni na Mambo Mengi..
Mhhhh  Unakumbuka Hii...Chei chei Shangazix2 Shangaziii shangazii...Uje Tena Shangazi x2 Tufurahi Shangazi Shangazii...

Jee wewe unamkumbuka nani na jee wewe ulikuwa Mpenzi wa kipindi Cha Watoto/Watoto Wetu/Chei Chei/MAMA NA MWANA?
Nini kingine ulichokuwa unakipenda kwenye kipi cha MAMA NA MWANA?
Hahahaha Tuma Salamu............

Nimatumaini Yangu Leo Mmefurahi sana.
Niwatakie JumaMosi Njema na Maendeleo mema ya EID.

Shukrani;http://hadithihadithi.podomatic.com/

Ni mimi Shangazi/Mama Yenu;Rachel [kachiki]

Wednesday 7 August 2013

Watoto na Michezo;Family Fun Day-Iliandaliwa na Hebron Church!!!!!!











Wazazi/Walezi na Watoto..Hii ilikuwa "Family Fun Day"..iliandaliwa na "Hebron Church"..Lakini haikuwa kwa Waumini/Washarika/Wakristo tuu..Japo waandaji ni Waumini/Waamini katika Kristo..Ilikuwa ya Watu wote,Ya wazi,Kwenye Viwanja[Park] kila mtu aliyependa kujumuika aliungana nasi/nao.
Ilikuwa ni  Kufurahi,Kucheza,Kula,Kujuana,Kujichnganya na Jamii..Pia kulikuwa na Kuchangia Watoto wenye shida..kama ulivyoona hapo juu kwenye Tangazo la[ZOE'S PLACE BABY HOSPICE] Na haikuwa lazima wewe kuchangia ndiyo ujumuike..kama uliguswa.. na kama siyo. Unaendelea Kujimwaga na Familia Yako.
Kulikuwa na Maswali mengi ya Watoto Wadadisi na kujifunza meengi....
Tulifurahi,Kujifunza,Kujuana,Kushirikiana Pamoja. kwani Mbele za MUNGU SOTE NI WAMOJA!!!

Wazazi/Walezi ni vyema tukajenga/kutenga nafasi ya kucheza pamoja na watoto wetu,wa Rafikiki zetu,Majirani na wengine.

 Asanteni sana na MUNGU azidi kutubariki soote...
Nkiripoti kutoka;STOKE GREEN[PARK],BINLEY ROAD.

Ni mimi;Mama/Shangazi Yenu,Rachel siwa[KACHIKI]