Thursday 28 February 2013

Mtoto Mchanga aokotwa Kimara Baruti!!!!!!


Wasamariawema wakimsafisha uchafu mtoto mchanga baada ya kumuokota  katika eneo la bondeni huko Kimara Baruti Bondeni karibu na maeneo ya Ubungo Kibangu.
Kitoto hicho baada ya kusafishwa na wasamaria wema 
Leo asubuhi wasamaria wema  wamekiokota kitoto kichanga cha kiume huko Kimara baruti  bondeni karibu na Ubungo kibangu , wasamaria hao baada ya kumsafisha uchafu na damu waliamua kumpeleka mtoto huyo kwenye hospital ya Palestina kwa huduma ya kwanza na baadae  Hospital ya Mwananyamala ambako kuna kitengo maalumu cha kuhudumia watoto wachanga . Baadhi ya watu walioshuhudia tukio hilo wamesema kuwa kuna uwezekano wa mtoto huyo kutupwa leo asubuhi na hii imetokana na mtoto huyo  kukutwa akiwa hai na uwepo wa damu mbichi mwilini mwake .


Shukrani;Chinga One Blog

Tuesday 26 February 2013

Historia kwa Watoto Wetu;Upande wa Pili wa Mwalimu!!!!



Wazazi/Walezi..unafahamu Historia yako hata ya Ukoo wako na Kuwahadithia Watoto WAKO?

Jee hii kwako unaionaje? karibu sana kwa MAONI/USHAURI.

Asante;CreativeGenesTZ


Tuesday 19 February 2013

Watoto na Maisha ya Mitaani;Msikilize Mtoto Hassan!!!!



Wazazi/walezi na Jamii kwa ujumla..nini Maoni/Ushauri wako?


Mama aliyemlisha Kinyesi na kumchoma moto mtoto ahukumiwa kifungo cha maisha jela!!!!!!

Wilvina Mkandala (24) akitolewa mahakamani mara tu baada ya kusomewa hukumu ya kifungo cha maisaha 
 Mtoto Aneth kabla ya kukatwa kwa mkono wake wa kushoto


Mtoto Aneth mara baada ya kukatwa mkono wa kushoto kwa ujumla mtoto huyu anaendelea vizuri na alishatoka hospitalini.



Na Ezekiel Kamanga, Mbeya.
WILIVINA MKANDALA mwenye umri wa miaka 24 ameukumiwa kutumikia kifungo cha maisha jela baada ya kukutwa na hatia ya kumlisha mtoto ANETH GASTO mwenye umri wa 5 mitano kinyesi na na kumuunguza kwa maji ya moto

Akisoma hati ya mashtaka mwendesha mashtaka wa serikali ACHIREY MULISA ameiomba mahakama hiyo kutoa adhabu kali kwa mshtakiwa ili iwe fundisho kwa watu wegine wenye tabia kama hiyo

Akisoma hukumu hiyo kwa muda wa dakika hamsini hakimu mfawidhi wa mahakama ya wilaya mbeya GILBERT NDEURUO ameridhishwa na   na ushahidi uliotolewa na upande  wa Jamuhuri kwamba  mshtakiwa amtenda kosa kinyume cha sheria  cha makosa ya jinai namba 222(a)sura  ya kumi na sita ya marekebisho ya mwaka 2002

Hata hivyo ameiomba serikali kutunga sheria ya kumlinda  mtoto kutokana na vitendo vilivyokithiri kwa  watoto ambapo amesema tanzania haina sheria ya kulinda mtoto

Akijitetea mahakamani mtuhumiwa huyo   ameiomba mahakama kumpunguzia adhabu kwani anategemewa na familia sababu ambazo zilipingwa na mahakama hiyo.

MTOTO MCHANGA AOKOTWA HUKO CHANIKA!!!!


Mtoto Mchanga Anayekadiriwa Kuwa na Mwezi Mmoja Amekutwa Ametupwa Na Mama Ambae Hadi sasa Hajafahamika.Mnamo tarehe 10-02-2013-saa kumi na Mbili jioni Eneo la Chanika Mtoto Huyo Aliokotwa Na Mohamedi Ramadhani Ambaye ni Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa na Kumpeleka Kituo Kidogo Cha Polisi Chanika.Ndipo Askari Wa Doria Ikawalazimu kumpeleka Mtoto huyo Hospitali ya Taifa ya Muhimbli Dar es Salam Kwahuduma Zaidi.

PICHA NA KHAMISI MUSSA)

Shukrani;KapingaZ Blog.

Friday 15 February 2013

Mtoto Siku Ya kwanza Shuleni!!!!!!


Wazazi/Walezi.;Ilikuwaje siku ya kwanza mtoto wako alipoanza Shule?..
Hii ilikuwa siku ya kwanza Shangazi yangu Sabrina kuanza Shule..

Mmmhh Ujanja wote mfukoni..ni Mpoleee..ngoja arudi Nyumbani hahaaa..

jee na wewe Unakumbuka siku yako ya kwanza Kuanza Shule?

Watoto Na Vituko/Utundu!!!


Watoto na Vituko/Utundu..kama hutaki kumpatia kitu anachotaka..si kwa ubaya..labda kinamfanya asiweze kula vyema na sababu nyingine...kwake yeye anaona kama unamnyima..

Yupo Tayari atafute mbinu zake ili afanikishe.....Vipi wewe Mzazi/Mlezi umekutana na haya?

Watoto na Hali ya Hewa ya Baridi !!!




Watoto huwa wanafurahia hali yoyote..ikiwa Baridi na Snow wao huwa wanafurahi sana.Ikiwa Jua ndiyo kabisaaa...