Friday 16 June 2017

Leo ni Siku ya Mtoto Wa Afrika;Mtoto UmlevyoNdivyo akuavyo..!
Shukrani;Tanzania Sci

Habari za siku nyingi watoto wangu wapendwa..
Natumaini wote mnaendelea vyema..
Mnisamehe kwa kuadimika huku ni majukumu yameingiliana..

Leo nimewakumbuka sana...
Nawatakia Siku hii njema ya Mtoto wa Afrika na mkawe watoto wema na mjivunie kuwa kati ya watoto wa Afrika popote ulipo..
Mimi mwenyewe najivunia mno kuwa mtoto wa Afrika hata kama kwa sasa siishi huko..
Kuna mambo mema mengi ya kujivunia Afrika..
Mungu anasababu ya sisi kuwa wa Aafrika..

Leo ngoja niishie hapa nitajitahidi kuwa nanyi wakati mwingine..

Nawapenda sana..
Wenu Mama/Shangazi;Rachel siwa[Kachiki]

Sunday 22 March 2015

TANZANIA CHILDREN'S PROJECT YAFANYA HARAMBEE KUSAIDIA WATOTO TANZANIA COLUMBIA, MARYLAND


Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Liberata Mulamula akihudhuria harambee ya Tanzania Children's Project inayoshughulisha na miradi ya afya na elimu Tanzania iliyofanyika siku ya Jumamosi March 21, 2015 Columbia, Maryland. Kulia ni Timothy Lynch ambaye ni Rais wa NGO hiyo, Mhe. Balozi Liberata Mulamula aliongozana na Afisa wa Ubalozi Switebert Mkama(pichani kushoto)
Rais wa Tanzania Children's Project Bwn. Timothy Lynch katika picha ya pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Liberata Mulamula.
Wadau mbalimbali waliohudhuria harambee ya Tanzania Children's Project iliyofanyika siku ya Jumamosi March 21, 2015 Columbia, Maryland nchini Marekani.
 
picha ya pamoja
Picha ya pamoja
 
Kikundi cha muziki kikitoa burudani.

Saturday 14 March 2015

Watoto Wetu Leo;Vibonzo Vinavyofurahisha Mioyo ya Watoto

Habari za siku nyingi wapenzi Wazazi/Walezi na Watoto...
Samahani nilipotea kidogo mambo yaliingiliana.
Natumaini mko salama na manaendelea vyema na masomo/maisha ya kila siku.

Basi nisiwachoshe Leo tujifunze Vibonzo/Katuni zinavoandaliwa..
Pia kupitia Vibonzo/katuni kuna mambo mengi ya kujifunza.

Twende pamoja sasa...Shukrani;william Ndunde

Ni mimi Shangazi/Mama yenu Rachel siwa[Kachiki] Nawataki Jumamosi Njema.

Saturday 6 December 2014

Watoto Wetu;Movie ya Leo-Baby Geniuses Baby Squad Investigators 2013;Burudani-Sing Gary Barlow & The Commonwealth Band featuring Military Wives-

Wapendwa waungwana;Wazazi/Walezi na Watoto,Nimatumaini yangu wote hamjambo na mnaendelea vyema katika maisha ya kila siku na maandalizi ya christmas.....
Basi msiache kutujuza maandalizi ya sikukuu hii hapo mlipo yanaendeleaje.....

Huku maandalizi yanaendelea vyema,watu wapo mbiombio sana kwa manunuzi ya zawadi na vitu vingine vingi.....
Hali ya hewa ni baridi kwa sasa lakini si tatizo kwa watu wa huku wanavaa makoti na manunuzi yanaendelea....

Basi nisiwachoshe,Tuungane kwa kuangalia Movie ya Leo.........thanks;lawrinynet

Burudani-

Sing - Gary Barlow & The Commonwealth Band featuring Military WivesNawatakia kila la heri na maandalizi mema ya sikukuu ya Christmas na Mwaka mpya..
Ni mimi mama/shangazi yenu Rachelsiwa[Kachiki].

Saturday 22 November 2014

Watoto Wetu;Movie Ya Leo-A Grandpa for Christmas....


Wapendwa;Wazazi/Walezi na Watoto,Natumaini wote hamjambo na mnaendelea vyema.
Jee mmeshaanza maandalizi ya Christmas?
Watoto wa Ng'ambo baridi imeshaanza na usiku unaingia mapema sana,Pia wakati huu si wakucheza nje.Poleni sana.
Watoto wa nyumbani Afrika/Tanzania na sehemu nyingine natumaini manaendelea vyema na shule,michezo!!!!

Basi nisiwachoshe,Leo tuangalie Movie hii ...Thanks;Bodo Kiss


Nawatakia mapumziko mema ya mwisho wa wiki,muendelee kuwa Waaminifu,Mpendane,Mshirikiane na Mfurahi pamoja....
Ni mimi Mama/Shangazi yenu Rachel siwa[Kachiki]Nawapenda wote
.