Saturday 30 August 2014

Watoto WetuMovie ya Leo;Frozen,Burudani-Kidz Bop Kids-The Edge Of Glory..!!!!!!

Watoto na Michezo,Raha Siku Ya "Family Fun Day"
Watoto wangu wapendwa,Wazazi/Walezi..Natumaini wote hamjambo..Poleni na Samahani kwa kupotea  kwangu..sikuwa na tatizo ni  mambo kidogo tuu yaliingiliana.
Tupo tena pamoja!!
Haya watoto wa Ng'ambo maandalizi ya kurudi masomoni yameanza.Tunawatakia maandalizi mema na mkafanye vyema.


Watoto wangu wa Afrika/Nyumbani natumaini mnaendelea vyema.
Wazazi/Walezi poleni na majukumu,Lakini yasiwe kikwazo cha kukosa muda wa kukaa,kucheza,kuongea,kufurahi,kufundisha,Kuelimisha na kusikiliza watoto wanapenda nini na kwa nini na hapendi nini na kwanini
?


Basi nisiwachoshe tuangalie Movie ya Leo....

Burudani....


Nawatakia kila lililojema na Baraka..
Ni mimi Shangazi/Mama Yenu Rachel siwa[Kachiki]

Saturday 9 August 2014

Watoto Wetu;Movie Ya Leo;Little Girl Lost (Full Movie)

Nimatumaini yangu Wazazi/Walezi na Watoto wangu wapendwa hamjambo na mnaendelea vyema.
Leo tuangalie;Little Girl Lost.....

 Thanks;
 MoviesAndDocumentaries
Nawatakia Kheri na Baraka Wazazi/Walezi na Watoto wooooote waliozaliwa mwezi huu wa 08.[August]
Nami ni mmoja wao nilisheherekea yangu tarehe 01.08.
Nawatakia Likizo njema kwa walio Likizo[Holiday]

Nawatakia mapumziko mema ya mwisho wa wiki.
Ni mimi Mama/Shangazi yenu Rachel siwa [Kachiki]

Friday 8 August 2014

Watoto Na Kujifunza; Wakati wa Likizo [Summer Holiday] Na Watoto Wetu!!!!!!

Wapendwa;Wazazi/Walezi na Watoto wangu wote,Natumai mnaendelea nyema.
Watoto wa Ng'ambo mnaendeleaje na Likizo?Nini mnafanya/mmefanya?
Likizo ya mwaka jana;Tulianza kukutana na watoto na kujifunza kushona Watoto wa Bandia[Mwana Sesere.]
Watoto wa Bandia  au [Wana Sesere] ndilo jina ninalojua/nilikuwa natumia enzi zangu..
Tena tulikuwa tunashona wenyewe..kwa msaada wa wakubwa,kama-Dada,Mama wadogo,Shangazi wadogo,Marafiki na....
Pia Tuliweza kutengeneza watoto[Wana Sesere] kwa kutumia udongo.
Kwakutumia Udongo ,Tulitengeneza Mgari,Vyungu na vitu vingi..
Hasa watoto wengi tulio zaliwa/kukulia Afrika tunajua hii..sina hakika na jina kama wote walikuwa wanaita hivyo..
Basi nami nikaona vyema niwafundishe na watoto wa ki-Afrika/Waswahili waishio Ng'ambo Kutengeneza/Kushona.
Hii ilikuwa Likizo ya Mwaka Jana.
Mwaka huu nitawaletea picha kidogo za "Family Fun Day"Tulikuwa na wakati mzuri sana, Tulikutana na kucheza pamoja kwenye park.


Je watoto wa leo/sasa Afrika bado mnashona/tengeneza mwanasesere?
Je watoto mnapenda michezo gani wakati huu wa Kiangazi/Jua[Summer]..?
Je Watoto wa Ng'ambo mnapenda kujifunza/kujua michezo ya zamani au ya watoto wa Afrika?

Basi nisiwachoshe,Tupatapo muda na tukutane pamoja kwa kucheza na kufurahi pamoja.
Nawatakia Likizo njema kwa wote mnaondelea na Likizo.Pia masomo mema kwa wote mnaondelea na masomo.


Ni mimi Mama/Shangazi yenu;Rachel siwa[kachiki].