Friday 28 June 2013

Saturday 22 June 2013

Watoto Wetu;Ndoto Yangu-Katuni;burudani-Martina Chambili,Tanzania Nakupenda!!!!!




Watoto,Wazazi/Walezi..kuna ayefahamu Martina yuko wapi na anafanya nini? jee anaendelea kuimba?

Jee haya yaliyoimbwa kwenye wimbo huu bado yapo kwa TANZANIA Yetu ya Leo?



Umejifunza nini kupitia Katuni hii?

Karibu wote!!!!!!

Thursday 20 June 2013

Watoto wetu na kujifunza yetu;da'Yasinta[KADALA] Anasema Mtoto umleavyo!!!!!!!!!!!!


KUJIFUNZA/KUJITEGEMEA MAISHA/KAZI ZA NYUMBANI!! AU MTOTO UMLEAVYO NDIVYO AKUAVYO!!



Tulipokuwa nyumbani mwezi wa sita mwishoni mpaka wa nane mwanzoni bahati nzuri ulikuwa ni msimu wa kuvuna. Tulimkuta Mzee ngonyani/babu amevuna mahindi. Na hapa mnamwona kijana Erik akimsaidia babu kupiga mahindi, kwa babu Songea Ruhuwiko.



Baada ya kazi nzito ya kupiga mahindi nguo zilikuwa zimechafuka kwa hiyo ni lazima kufua na hapa mnamwona anafua nguo zake....hapa ni Songea Ruhuwiko ....


Dada mtu naye siku yake ya dobi ikaja kama mnavyoona naye anafua nguo zake. Hii /hizi kazi ni moja ya kujifunza kuishi kwa kujitegemea.Uzuri wake maji tulikuwa nayo humu humu uani.


MAISHA NI KUJIFUNZA.
imeandikwa na da'yasinta [Kadala]wa;http://ruhuwiko.blogspot.co.uk/

Friday 14 June 2013

Watoto Na Malezi;Da'Tolly Tolly Anauliza;UNALEA WATOTO AU MAYAI?KESHO YAO ITAKUAJE?




043
Katika maisha si kila unalolifanya unafanya kwasababu unapenda au unafurahia, wakati mwingine maisha yanatulazimu kufanya mambo Fulani au kujua jambo Fulani kwasababu ni muhimu kwetu au kwasababu jamii inatutaka tujue na kuweza.
Kupika ni moja ya hayo. si kila mtu anapenda kupika, lakini ualisia wa maisha unawalazimu  watu kujua kupika.Kwa maisha yetu ya kiafrika kujua kupika ni jambo la lazima kwa mwanamke,hata ivyo ualisia wa mabadiliko ya maisha karne hii ya 21 yanawalazimu hata wanaume kujua kupika.
Kupika ni jambo la kujifunza kwa wazazi na ndugu wanaokuzunguka katika kukua kwake,ni kitu unachojifunza kila siku ya maisha yako na kwakufanya mazoezi ya kupika mara kwa mara kama sehem ya ushiriki wa kazi za nyumbani.
Wazazi wa siku hizi wanawanyima watoto  nafasi ya kujifunza kupika kwa kushiriki kazi za nyumbani.Familia nyingi zina dada au kaka anaefanya kazi zote za ndani na matokeo yake watoto wengi hufanya kazi ya kuangalia Tv siku nzima na kukaa kwenye viti kama mayai  kwenye trei.
Kuwalea watoto wako kama mayai,kutowashirikisha katika kazi za nyumbani na shughuli zako za biashara na mambo mengine ni kosa kubwa sana.Ni kumnyima mtoto nafasi ya kujifunza mambo mbalimbali yampasayo kujua kwenye maisha.
Huku jikoni mtoto anatakiwa kushiki kazi ndugo ndogo tangu anapokua mdogo,aanze kwa kutoan vyombo mezani,kufuta meza,kupanga meza,kufagia jiko,kutwanga vitunguu swaumu na mambo madogo madogo kama hayo kutokana na umri wake.
Hapo nyumbani wapangie watoto zamu na taratibu za kufanya kazi za nyumbani.si kupika tu,bali kazi za nyumbani kwa ujumla.
Tulipokuwa wadogo,mama yetu alitupangia zamu na ratiba ya kazi zote,kutofanya kazi katika wakati husika kuliambatana na adhabu ya kufanya kazi hiyo kwa siku tatu  mfululizo kama kazi ya nyongeza,uku wengine wakipumzika.Ratiba ya kazi hizi ilibandikwa nyuma ya mlango wa kabati  jikoni na ilizingatia umri.Ratiba yetu likua na mambo haya:
1.Ratiba ya kuamka kuandaa chai asubuhi
2.Ratiba ya kupika  mchana na usiku
3.Ratiba ya kuosha vyombo,wadogo wanaosha vyombo vya chai asubuhi
4.Ratiba ya kupanga meza(wadogo)
5.Ratiba ya kufuta meza(wadogo)
6.Ratiba ya kusafisha Sebule na jiko
7.Ratiba ya kusafisha vyumba
8.Ratiba ya kusafisha choo na bafu
9.Ratiba ya kufagia nje
10.Ratiba ya kumwagilizia mauwa
11.Ratiba ya kumsaidia mama kwenye biashara
12.Zamu ya kusali na kuongoza ibada ya jioni
042
Zaidi ya ratiba kulikua na kanuni au sharia ambazo zilikua lazima kufuata na kila moja ilikua na adhabu yake pale unapoivunja.
1.Lazima kuoga kabla ya kwenda mezani kupata kifungua kinywa na kabla ya kwenda kupata chakula cha jioni.Usipooga basi hakuna kwenda mezani,ikimaanisha hautakula.
2.Lazima kufua nguo na kupanga kabati kila jumamosi.Usipofanya hivyo jumapili wengine wakipelekwa kutembea,wewe unabaki nyumbani .
3.Home work zote lazima zifanywe kabla ya saa moja jioni,na umpe mama,baba,mtu mkubwa yoyote akague .Usipofanya hivyo mara nyingi adhabu ilikua kufanya maswali mengine kumi kama hayo au anamwambia mwalimu wako akushugulikie shuleni.
4.Kwenda kanisani ni lazima,hili halikua na mjadala na hakukua na namna ya kulikwepa.
5.Hakuna kuangalia Tv wala sinema kabla ya saa nane mchana.Asubuhi ni walkati wa kazi,mapumziko ni Baada ya  Lunch.Adhabu ya kuvunja hili ilikua ni kupewa kazi za kufanya,kwani kukaa unaangalia Tv maana yake huna kazi.Unaambiwa kashone vifungo vilivyotoka kwenye nguo zako,au kafute na kubrashi viatu vyako.
  • Hizi ni baadhi ya ratiba na sharia au kanuni zilizonilea,na kunifanya niwe hivi nilivyo leo.ratiba hizi zilihusisha watoto wote,wakiume na wakike.Kwa ratiba kama hizi mtoto anajifunza kila kitu  na anajifunza kujitegemea kwa kila kitu.
Ifike mahala muone aibu na mjiulize watoto wenu watakua kina baba au kina mama wanamna gani wakikua.Waswahili husema  Samaki mkunje  angali mbichi.Wewe unaengoja Samaki wako aive ndipo umkunje,utatia aibu na utaumbuka.
Pia ni vyema kujua kuwa,ni katika ufanyaji wa kazi hizi unaanza kuona na kutambua uwezo na vipaji vya watoto.Mpishi mzuri utaanza kumuona mapema,wale wanaopenda kusimamia wenzao ndio vipaji vya uongozi hivyo,kuna wale wa maneno mengi ila hawafanyi kazi nao utawajua na uanze kuwasaidia kubadili tabia hizo zisizofaa.
Hapa jikoni watoto wakija lazima niwape kazi yakufanya,kama hakuna kazi basi nampa kiti akae mlangoni(kukwepa ajali) tuongee mawili matatu wakati napika.Kwani najua anapoangalia niachofanya kula jambo anajifunza,na mara nyingi wanakua na maswali mengi juuu ya lile ninalolifanya.
Yangu ni haya tu kwa leo,yaliyobaki kazi kwako.Ukiamua kulea watoto kama mayai  basi endelea ukijua unamuharibia mtoto maisha.
kwa mambo ya mapishi na malezi ingia hapa;http://tollyzkitchen.wordpress.com/

Wednesday 12 June 2013

Kueleke Siku Ya Mtoto Wa Afrika; Wazo La Leo na Emu-Three!!!!!!





WAZO LA LEO:,Kumbuka ipo siku maalumu, inayotambulikana kama ya siku ya mtoto wa Afrika tarehe 16 June, sijui kama upo makini na siku hii, huenda kwako ni historia tu ya Mauaji ya Soweto…kwani unaishi kwenye kisiwa cha amani, huna shida…una kazi nzuri, gari..nk. Lakini kumbuka kuna hawa watoto wa mitaani, unawakumbuka?

 Je siku ya mtoto kwako inakugusaje?


Je wewe kama mzazi, unahisije ukiwaona watoto wa mitaani, au ndio huko kusema, `hawa watoto wanaomba omba tu, hawaendi shule…' hawa kwa mateso wanayoyapata hawana tofauti na wale watoto waliouwawa kikatili,…..wewe hutumii, silaha, lakini unatumia njia nyingine, isiyoonekana, ya kutokutimiza wajibu wako kama mzazi.


Kumbuka mateso wanayopata hawa watoto, kwanza kisaikolojia pale wanapoona wenzao wakiwa kwenye sare za shule, au wakipita na magari wakiepelekwa mashuleni.  Lakini pia kuwa mateso ya afya zao, kwani wengine wanaishia majalalani kuokota yale mabaki ya vyakula mliyokula na kusaza. Huyu ni mtoto wako hata kama hukumzaa wewe, kumbukeni kila mtoto ana mzazi, na mzazi wake ni mimi na wewe.

Imeandikwa na emu-three wa Diary Yangu.



Zaidi ingia kwa ndugu wa mimi,Pia kwa Visa vya kusisimua na Mambo meengi;http://miram3.blogspot.co.uk/







--
Posted By Blogger to Swahili na Waswahili on 6/12/2013 12:12:00 pm