Saturday, 22 November 2014

Watoto Wetu;Movie Ya Leo-A Grandpa for Christmas....


Wapendwa;Wazazi/Walezi na Watoto,Natumaini wote hamjambo na mnaendelea vyema.
Jee mmeshaanza maandalizi ya Christmas?
Watoto wa Ng'ambo baridi imeshaanza na usiku unaingia mapema sana,Pia wakati huu si wakucheza nje.Poleni sana.
Watoto wa nyumbani Afrika/Tanzania na sehemu nyingine natumaini manaendelea vyema na shule,michezo!!!!

Basi nisiwachoshe,Leo tuangalie Movie hii ...



Thanks;Bodo Kiss


Nawatakia mapumziko mema ya mwisho wa wiki,muendelee kuwa Waaminifu,Mpendane,Mshirikiane na Mfurahi pamoja....
Ni mimi Mama/Shangazi yenu Rachel siwa[Kachiki]Nawapenda wote
.

Saturday, 27 September 2014

Watoto Wetu Leo;African storytelling na ZinseAgginie,Burudani-HukweZawose!!!!!!!

Wazazi/Walezi na Watoto wangu Wapendwa,Nimatumaini yangu wote hamjambo na mnaendelea vyema..kwa wale wagonjwa,wenye matatizo yoyote..tuwaombea mpate kupona na kupata utatuzi wa mapito yote,Mungu yu pamoja nanyi.....
Hapa tulipo hali ya hewa imebadirika kwa sasa,(Autumn)...Watoto wa huku watakosa kucheza nje.
Vipi hapo ulipo wewe?

Basi nisiwachoshe Leo tuungane na Zinse kwa Hadith nzuri .......


Shukrani/Thanks;zinse agginie

Burudani na Hukwe Zawose


Nawatakia weekend njema,yenye Upendo,Umoja na Afya njema....


Ni Mimi Shangazi/Mama yenu Rachel siwa[Kachiki]
Tukutane pale kwa Mwalimu,Baba,Babu,Mtumishi - Mwakasege
Yupo Hapa Coventry,UK
 


Saturday, 13 September 2014

Watoto wetu Leo tujifunze kuhusu Mwalimu Julius Nyerere[Baba wa TaifaLa Tanzania]

Nimatumaini yangu Wazazi/Walezi na Watoto wangu wapendwa wote hamjambo na mnaendelea vyema.
Watoto leo tujifunze kuhusu Baba wa Taifa la Tanzania..Mwalimu Julius Nyerere....

Natumaini mtajifunza mengi kuhusu Baba wa Taifa..
Twende pamoja......


Shukrani/Thanks;CCTV Africa

Nawatakia mapumziko mema ya mwishoni mwa wiki...
Ni mimi Mama/Shangazi yenu Rachel siwa[Kachiki]
 

Saturday, 30 August 2014

Watoto WetuMovie ya Leo;Frozen,Burudani-Kidz Bop Kids-The Edge Of Glory..!!!!!!

Watoto na Michezo,Raha Siku Ya "Family Fun Day"
Watoto wangu wapendwa,Wazazi/Walezi..Natumaini wote hamjambo..Poleni na Samahani kwa kupotea  kwangu..sikuwa na tatizo ni  mambo kidogo tuu yaliingiliana.
Tupo tena pamoja!!
Haya watoto wa Ng'ambo maandalizi ya kurudi masomoni yameanza.Tunawatakia maandalizi mema na mkafanye vyema.


Watoto wangu wa Afrika/Nyumbani natumaini mnaendelea vyema.
Wazazi/Walezi poleni na majukumu,Lakini yasiwe kikwazo cha kukosa muda wa kukaa,kucheza,kuongea,kufurahi,kufundisha,Kuelimisha na kusikiliza watoto wanapenda nini na kwa nini na hapendi nini na kwanini
?


Basi nisiwachoshe tuangalie Movie ya Leo....

Burudani....


Nawatakia kila lililojema na Baraka..
Ni mimi Shangazi/Mama Yenu Rachel siwa[Kachiki]