Friday 8 August 2014

Watoto Na Kujifunza; Wakati wa Likizo [Summer Holiday] Na Watoto Wetu!!!!!!

Wapendwa;Wazazi/Walezi na Watoto wangu wote,Natumai mnaendelea nyema.
Watoto wa Ng'ambo mnaendeleaje na Likizo?Nini mnafanya/mmefanya?
Likizo ya mwaka jana;Tulianza kukutana na watoto na kujifunza kushona Watoto wa Bandia[Mwana Sesere.]
Watoto wa Bandia  au [Wana Sesere] ndilo jina ninalojua/nilikuwa natumia enzi zangu..
Tena tulikuwa tunashona wenyewe..kwa msaada wa wakubwa,kama-Dada,Mama wadogo,Shangazi wadogo,Marafiki na....
Pia Tuliweza kutengeneza watoto[Wana Sesere] kwa kutumia udongo.
Kwakutumia Udongo ,Tulitengeneza Mgari,Vyungu na vitu vingi..
Hasa watoto wengi tulio zaliwa/kukulia Afrika tunajua hii..sina hakika na jina kama wote walikuwa wanaita hivyo..
Basi nami nikaona vyema niwafundishe na watoto wa ki-Afrika/Waswahili waishio Ng'ambo Kutengeneza/Kushona.
Hii ilikuwa Likizo ya Mwaka Jana.
Mwaka huu nitawaletea picha kidogo za "Family Fun Day"Tulikuwa na wakati mzuri sana, Tulikutana na kucheza pamoja kwenye park.


Je watoto wa leo/sasa Afrika bado mnashona/tengeneza mwanasesere?
Je watoto mnapenda michezo gani wakati huu wa Kiangazi/Jua[Summer]..?
Je Watoto wa Ng'ambo mnapenda kujifunza/kujua michezo ya zamani au ya watoto wa Afrika?

Basi nisiwachoshe,Tupatapo muda na tukutane pamoja kwa kucheza na kufurahi pamoja.
Nawatakia Likizo njema kwa wote mnaondelea na Likizo.Pia masomo mema kwa wote mnaondelea na masomo.


Ni mimi Mama/Shangazi yenu;Rachel siwa[kachiki].

No comments: