Friday, 16 June 2017

Leo ni Siku ya Mtoto Wa Afrika;Mtoto UmlevyoNdivyo akuavyo..!




Shukrani;Tanzania Sci

Habari za siku nyingi watoto wangu wapendwa..
Natumaini wote mnaendelea vyema..
Mnisamehe kwa kuadimika huku ni majukumu yameingiliana..

Leo nimewakumbuka sana...
Nawatakia Siku hii njema ya Mtoto wa Afrika na mkawe watoto wema na mjivunie kuwa kati ya watoto wa Afrika popote ulipo..
Mimi mwenyewe najivunia mno kuwa mtoto wa Afrika hata kama kwa sasa siishi huko..
Kuna mambo mema mengi ya kujivunia Afrika..
Mungu anasababu ya sisi kuwa wa Aafrika..

Leo ngoja niishie hapa nitajitahidi kuwa nanyi wakati mwingine..

Nawapenda sana..
Wenu Mama/Shangazi;Rachel siwa[Kachiki]

Sunday, 22 March 2015

TANZANIA CHILDREN'S PROJECT YAFANYA HARAMBEE KUSAIDIA WATOTO TANZANIA COLUMBIA, MARYLAND


Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Liberata Mulamula akihudhuria harambee ya Tanzania Children's Project inayoshughulisha na miradi ya afya na elimu Tanzania iliyofanyika siku ya Jumamosi March 21, 2015 Columbia, Maryland. Kulia ni Timothy Lynch ambaye ni Rais wa NGO hiyo, Mhe. Balozi Liberata Mulamula aliongozana na Afisa wa Ubalozi Switebert Mkama(pichani kushoto)
Rais wa Tanzania Children's Project Bwn. Timothy Lynch katika picha ya pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Liberata Mulamula.
Wadau mbalimbali waliohudhuria harambee ya Tanzania Children's Project iliyofanyika siku ya Jumamosi March 21, 2015 Columbia, Maryland nchini Marekani.
 
picha ya pamoja
Picha ya pamoja
 
Kikundi cha muziki kikitoa burudani.

Saturday, 14 March 2015

Watoto Wetu Leo;Vibonzo Vinavyofurahisha Mioyo ya Watoto

Habari za siku nyingi wapenzi Wazazi/Walezi na Watoto...
Samahani nilipotea kidogo mambo yaliingiliana.
Natumaini mko salama na manaendelea vyema na masomo/maisha ya kila siku.

Basi nisiwachoshe Leo tujifunze Vibonzo/Katuni zinavoandaliwa..
Pia kupitia Vibonzo/katuni kuna mambo mengi ya kujifunza.

Twende pamoja sasa...



Shukrani;william Ndunde

Ni mimi Shangazi/Mama yenu Rachel siwa[Kachiki] Nawataki Jumamosi Njema.

Saturday, 6 December 2014

Watoto Wetu;Movie ya Leo-Baby Geniuses Baby Squad Investigators 2013;Burudani-Sing Gary Barlow & The Commonwealth Band featuring Military Wives-

Wapendwa waungwana;Wazazi/Walezi na Watoto,Nimatumaini yangu wote hamjambo na mnaendelea vyema katika maisha ya kila siku na maandalizi ya christmas.....
Basi msiache kutujuza maandalizi ya sikukuu hii hapo mlipo yanaendeleaje.....

Huku maandalizi yanaendelea vyema,watu wapo mbiombio sana kwa manunuzi ya zawadi na vitu vingine vingi.....
Hali ya hewa ni baridi kwa sasa lakini si tatizo kwa watu wa huku wanavaa makoti na manunuzi yanaendelea....

Basi nisiwachoshe,Tuungane kwa kuangalia Movie ya Leo.........



thanks;lawrinynet

Burudani-

Sing - Gary Barlow & The Commonwealth Band featuring Military Wives



Nawatakia kila la heri na maandalizi mema ya sikukuu ya Christmas na Mwaka mpya..
Ni mimi mama/shangazi yenu Rachelsiwa[Kachiki].

Saturday, 22 November 2014

Watoto Wetu;Movie Ya Leo-A Grandpa for Christmas....


Wapendwa;Wazazi/Walezi na Watoto,Natumaini wote hamjambo na mnaendelea vyema.
Jee mmeshaanza maandalizi ya Christmas?
Watoto wa Ng'ambo baridi imeshaanza na usiku unaingia mapema sana,Pia wakati huu si wakucheza nje.Poleni sana.
Watoto wa nyumbani Afrika/Tanzania na sehemu nyingine natumaini manaendelea vyema na shule,michezo!!!!

Basi nisiwachoshe,Leo tuangalie Movie hii ...



Thanks;Bodo Kiss


Nawatakia mapumziko mema ya mwisho wa wiki,muendelee kuwa Waaminifu,Mpendane,Mshirikiane na Mfurahi pamoja....
Ni mimi Mama/Shangazi yenu Rachel siwa[Kachiki]Nawapenda wote
.

Saturday, 27 September 2014

Watoto Wetu Leo;African storytelling na ZinseAgginie,Burudani-HukweZawose!!!!!!!

Wazazi/Walezi na Watoto wangu Wapendwa,Nimatumaini yangu wote hamjambo na mnaendelea vyema..kwa wale wagonjwa,wenye matatizo yoyote..tuwaombea mpate kupona na kupata utatuzi wa mapito yote,Mungu yu pamoja nanyi.....
Hapa tulipo hali ya hewa imebadirika kwa sasa,(Autumn)...Watoto wa huku watakosa kucheza nje.
Vipi hapo ulipo wewe?

Basi nisiwachoshe Leo tuungane na Zinse kwa Hadith nzuri .......


Shukrani/Thanks;zinse agginie

Burudani na Hukwe Zawose


Nawatakia weekend njema,yenye Upendo,Umoja na Afya njema....


Ni Mimi Shangazi/Mama yenu Rachel siwa[Kachiki]
Tukutane pale kwa Mwalimu,Baba,Babu,Mtumishi - Mwakasege
Yupo Hapa Coventry,UK
 


Saturday, 13 September 2014

Watoto wetu Leo tujifunze kuhusu Mwalimu Julius Nyerere[Baba wa TaifaLa Tanzania]

Nimatumaini yangu Wazazi/Walezi na Watoto wangu wapendwa wote hamjambo na mnaendelea vyema.
Watoto leo tujifunze kuhusu Baba wa Taifa la Tanzania..Mwalimu Julius Nyerere....

Natumaini mtajifunza mengi kuhusu Baba wa Taifa..
Twende pamoja......


Shukrani/Thanks;CCTV Africa

Nawatakia mapumziko mema ya mwishoni mwa wiki...
Ni mimi Mama/Shangazi yenu Rachel siwa[Kachiki]
 

Saturday, 30 August 2014

Watoto WetuMovie ya Leo;Frozen,Burudani-Kidz Bop Kids-The Edge Of Glory..!!!!!!

Watoto na Michezo,Raha Siku Ya "Family Fun Day"
Watoto wangu wapendwa,Wazazi/Walezi..Natumaini wote hamjambo..Poleni na Samahani kwa kupotea  kwangu..sikuwa na tatizo ni  mambo kidogo tuu yaliingiliana.
Tupo tena pamoja!!
Haya watoto wa Ng'ambo maandalizi ya kurudi masomoni yameanza.Tunawatakia maandalizi mema na mkafanye vyema.


Watoto wangu wa Afrika/Nyumbani natumaini mnaendelea vyema.
Wazazi/Walezi poleni na majukumu,Lakini yasiwe kikwazo cha kukosa muda wa kukaa,kucheza,kuongea,kufurahi,kufundisha,Kuelimisha na kusikiliza watoto wanapenda nini na kwa nini na hapendi nini na kwanini
?


Basi nisiwachoshe tuangalie Movie ya Leo....

Burudani....


Nawatakia kila lililojema na Baraka..
Ni mimi Shangazi/Mama Yenu Rachel siwa[Kachiki]

Saturday, 9 August 2014

Watoto Wetu;Movie Ya Leo;Little Girl Lost (Full Movie)

Nimatumaini yangu Wazazi/Walezi na Watoto wangu wapendwa hamjambo na mnaendelea vyema.
Leo tuangalie;Little Girl Lost.....

 Thanks;
 MoviesAndDocumentaries
Nawatakia Kheri na Baraka Wazazi/Walezi na Watoto wooooote waliozaliwa mwezi huu wa 08.[August]
Nami ni mmoja wao nilisheherekea yangu tarehe 01.08.
Nawatakia Likizo njema kwa walio Likizo[Holiday]

Nawatakia mapumziko mema ya mwisho wa wiki.
Ni mimi Mama/Shangazi yenu Rachel siwa [Kachiki]

Friday, 8 August 2014

Watoto Na Kujifunza; Wakati wa Likizo [Summer Holiday] Na Watoto Wetu!!!!!!

Wapendwa;Wazazi/Walezi na Watoto wangu wote,Natumai mnaendelea nyema.
Watoto wa Ng'ambo mnaendeleaje na Likizo?Nini mnafanya/mmefanya?
Likizo ya mwaka jana;Tulianza kukutana na watoto na kujifunza kushona Watoto wa Bandia[Mwana Sesere.]
Watoto wa Bandia  au [Wana Sesere] ndilo jina ninalojua/nilikuwa natumia enzi zangu..
Tena tulikuwa tunashona wenyewe..kwa msaada wa wakubwa,kama-Dada,Mama wadogo,Shangazi wadogo,Marafiki na....
Pia Tuliweza kutengeneza watoto[Wana Sesere] kwa kutumia udongo.
Kwakutumia Udongo ,Tulitengeneza Mgari,Vyungu na vitu vingi..
Hasa watoto wengi tulio zaliwa/kukulia Afrika tunajua hii..sina hakika na jina kama wote walikuwa wanaita hivyo..
Basi nami nikaona vyema niwafundishe na watoto wa ki-Afrika/Waswahili waishio Ng'ambo Kutengeneza/Kushona.
Hii ilikuwa Likizo ya Mwaka Jana.
Mwaka huu nitawaletea picha kidogo za "Family Fun Day"Tulikuwa na wakati mzuri sana, Tulikutana na kucheza pamoja kwenye park.


Je watoto wa leo/sasa Afrika bado mnashona/tengeneza mwanasesere?
Je watoto mnapenda michezo gani wakati huu wa Kiangazi/Jua[Summer]..?
Je Watoto wa Ng'ambo mnapenda kujifunza/kujua michezo ya zamani au ya watoto wa Afrika?

Basi nisiwachoshe,Tupatapo muda na tukutane pamoja kwa kucheza na kufurahi pamoja.
Nawatakia Likizo njema kwa wote mnaondelea na Likizo.Pia masomo mema kwa wote mnaondelea na masomo.


Ni mimi Mama/Shangazi yenu;Rachel siwa[kachiki].

Saturday, 19 July 2014

Watoto Wetu Leo;Movie ya Leo-Life-Size (2000) Full Movie. [Family Fun Day 02/08/14]

Wazazi/Walezi na Watoto wangu wapendwa;Nimatumaini yangu wote mnaendelea vyema.
Kwa wale wanaofunga poleni na Swaum[Ramadhani njema].
Watoto hapa UK /Ng'ambo Mmeanza Likizo na tunategema itakuwa nzuri na yenye kujifunza meengi,Bila kusahau kusaidia kazi za nyumbani na kusaidiana na wazazi/walezi kwa yale mnaoyaweza na kujifunza zaidi.....

Watoto,Wazazi/Walezi Mnaoshi hapa.... 
COVENTRY.UK.Msisahau "Family Fun Day"02/08/14
"Family Fun Day" zaidi itakuwa Michezo;Kuchora,Kuimba,Kucheza,Mitindo,Kuangalia Vipaji vya Watoto wetu,Kula na Kufurahi Pamoja... na Watoto.Na Mengine Meengi!!!!

Kwa maelezo zaidi;Email;rasca@hotmail.co.uk.
Mobile;0750 44 100 40.



Nawatakia Likizo Njema,Ramadhani Njema,Mnaondelea na Masomo Masomo Mema.


Ni Mimi Mama/Shangazi yenu;Rachel siwa[Kachiki]

Tuesday, 15 July 2014

Hongera sana da'Sandra-Neema ; Siku kama ya Leo Alizaliwa!!!!!










Hongera sana da'Sandra-Neema katika siku yako hii  Muhimu.
Hongera kwa kumaliza vyema GCSE's Na tunakitakia kila la heri katika A-Levels[Sixth Form].Ukawe kichwa na si Mkia.
Tunakupenda Sana na Tunakuunga mkono katika Safari yako njema ya Maisha.
MUNGU ndiyo kila kitu katika Maisha yako.Ubarikiwe Mno!!!!


Happy birthday Sandra-Neema!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!


Wako;Mama,Baba,Mdogo wako-Tracey-Sarah.[Isaac Family]
MUNGU wetu ni Mwema Sana.



#IsaacRachel#IsaacFamily#Tunawapenda Wote.



Saturday, 12 July 2014

Watoto Wetu Leo;Watoto Wamejifunza nini Kupitia-Ubongo Kids ? - Sisi Watoto Part 1- 2 - Tanzanian Cartoon..!!!!!

Hamjambo Wazazi/Walezi Na Watoto wangu Wapendwa?
Leo tuangalie Watoto wamejifunza,Kufaidikaje kupitia Ubongo Kids?






Je wewe umejifunza nini kupitia Ubongo Kids?

Shukrani Sana;Ubongo Kids
 Nawatakia Mapumziko mema na Muwe Watoto Wema.
Ni mimi Shangazi/Mama yenu;Rachel siwa[Kachiki]

Wednesday, 25 June 2014

Watoto Na Kujifunza;Jikoni Leo-How to make Chapati by Camila and Minza

Wazazi/Walezi na Watoto wangu wapendwa......
Watoto wetu na kujifunza mambo mbalimbali ya kwetu/Yaliyo na Manufaa kwao Pia ni sehemu ya kufurahi pamoja na wazazi/walezi,Kuwafunza na wenzao.

Jikoni Leo tunao kinadada wadogo wa Ki-Tanzania wanaoishi Marekani[USA].
"da'Camila na da'Minza"

wanatupikia CHAPATI....

Ungana nao nawe ujifunze kupitia wao..........


Je nini umejifunza kupitia Watoto hawa?
Je nawe una picha,Video unapenda kushiriki nasi?


Tuma kupitia;rasca@hotmail.co.uk.

Kumbuka;"Family Fun Day 02'08'2014"


Shukrani;iskajojophotography .

Saturday, 21 June 2014

Watoto Wetu Leo;Katuni/Vibonzo(Cartoons)Ubongo Kids Webisode 17-18 - Wakati ni Mali Part 1-2


"Family Fun Day" 02'08'14

Wazazi/Walezi na Watoto wangu wapendwa,Natumaini wote hamjambo na mnaendelea vyema.
Watoto wa Afrika,Tanzania Manaendeleaje na Likizo?
Je nini mmefanya/mnafanya wakati huu?

Watoto wa Ng'ambo naona mnafurahia Jua[Summer]
Msikose kwenye "Family Fun Day "02'08'14
 Jee mpo Tayari?


;https://www.facebook.com/events/Watoto na Jamii

Basi Nisiwachoshe,TuangalieKatuni Ya Leo Kutoka kwa Ubongo Kids Yenye Mafundisho.........







   Shukrani/Thanks;Ubongo Kids

Ni Mimi Mama/Shangazi yenu Rachel siwa[Kachiki]



Friday, 13 June 2014

Watoto Na Mitindo Yao;Summer Collection;[Maandalizi Ya Family Fun Day]!!!!!!!




Hamjambo Wazazi/Walezi na Watoto wangu Wapendwa?  Summer Time....Wakati wa Jua umewadia,Hiki ni kipindi kizuri sana hapa Ng'ambo kwa Michezo ya Nje,Unaweza kuvaa vizuri na si nguo nyiingi yaani makoti,Masweta na.......Pia kunakuwa na Likizo[Summer Holiday]......
Maandalizi Ya
 "Family Fun Day" zaidi itakuwa Michezo;Kuchora,Kuimba,Kucheza,Mitindo,Kuangalia Vipaji vya Watoto wetuNyama Choma,na VyaKula vingine, Kufurahi Pamoja... na Watoto.
Jee mpo Tayari?
Wengi huwa wanakwenda Likizo Afrika na sehemu nyingine kwa wale watakao kuwepo kwa mwaka huu tutafanya tukutane na kucheza pamoja.
Itakuwa baada ya mfungo wa Ramadhani ili na wote tufurahi pamoja.Inaweza kuwa Tarehe 02/08 panapo Majaaliwa.

Kama kuna Ushauri,Msaada katika kuandaa na Mengine yote,Usisite kuwasiliana nami.
Email;rasca@hotmail.co.uk.
Simu;0750 44 100 40.

Wote Mnakaribishwa katika Yote.

Ni mimi Mama/Shangazi yenu Rachel siwa[Kachiki].