Katika maisha si kila unalolifanya unafanya kwasababu unapenda au unafurahia, wakati mwingine maisha yanatulazimu kufanya mambo Fulani au kujua jambo Fulani kwasababu ni muhimu kwetu au kwasababu jamii inatutaka tujue na kuweza.
Kupika ni moja ya hayo. si kila mtu anapenda kupika, lakini ualisia wa maisha unawalazimu watu kujua kupika.Kwa maisha yetu ya kiafrika kujua kupika ni jambo la lazima kwa mwanamke,hata ivyo ualisia wa mabadiliko ya maisha karne hii ya 21 yanawalazimu hata wanaume kujua kupika.
Kupika ni jambo la kujifunza kwa wazazi na ndugu wanaokuzunguka katika kukua kwake,ni kitu unachojifunza kila siku ya maisha yako na kwakufanya mazoezi ya kupika mara kwa mara kama sehem ya ushiriki wa kazi za nyumbani.
Wazazi wa siku hizi wanawanyima watoto nafasi ya kujifunza kupika kwa kushiriki kazi za nyumbani.Familia nyingi zina dada au kaka anaefanya kazi zote za ndani na matokeo yake watoto wengi hufanya kazi ya kuangalia Tv siku nzima na kukaa kwenye viti kama mayai kwenye trei.
Kuwalea watoto wako kama mayai,kutowashirikisha katika kazi za nyumbani na shughuli zako za biashara na mambo mengine ni kosa kubwa sana.Ni kumnyima mtoto nafasi ya kujifunza mambo mbalimbali yampasayo kujua kwenye maisha.
Huku jikoni mtoto anatakiwa kushiki kazi ndugo ndogo tangu anapokua mdogo,aanze kwa kutoan vyombo mezani,kufuta meza,kupanga meza,kufagia jiko,kutwanga vitunguu swaumu na mambo madogo madogo kama hayo kutokana na umri wake.
Hapo nyumbani wapangie watoto zamu na taratibu za kufanya kazi za nyumbani.si kupika tu,bali kazi za nyumbani kwa ujumla.
Tulipokuwa wadogo,mama yetu alitupangia zamu na ratiba ya kazi zote,kutofanya kazi katika wakati husika kuliambatana na adhabu ya kufanya kazi hiyo kwa siku tatu mfululizo kama kazi ya nyongeza,uku wengine wakipumzika.Ratiba ya kazi hizi ilibandikwa nyuma ya mlango wa kabati jikoni na ilizingatia umri.Ratiba yetu likua na mambo haya:
1.Ratiba ya kuamka kuandaa chai asubuhi
2.Ratiba ya kupika mchana na usiku
3.Ratiba ya kuosha vyombo,wadogo wanaosha vyombo vya chai asubuhi
4.Ratiba ya kupanga meza(wadogo)
5.Ratiba ya kufuta meza(wadogo)
6.Ratiba ya kusafisha Sebule na jiko
7.Ratiba ya kusafisha vyumba
8.Ratiba ya kusafisha choo na bafu
9.Ratiba ya kufagia nje
10.Ratiba ya kumwagilizia mauwa
11.Ratiba ya kumsaidia mama kwenye biashara
12.Zamu ya kusali na kuongoza ibada ya jioni
Zaidi ya ratiba kulikua na kanuni au sharia ambazo zilikua lazima kufuata na kila moja ilikua na adhabu yake pale unapoivunja.
1.Lazima kuoga kabla ya kwenda mezani kupata kifungua kinywa na kabla ya kwenda kupata chakula cha jioni.Usipooga basi hakuna kwenda mezani,ikimaanisha hautakula.
2.Lazima kufua nguo na kupanga kabati kila jumamosi.Usipofanya hivyo jumapili wengine wakipelekwa kutembea,wewe unabaki nyumbani .
3.Home work zote lazima zifanywe kabla ya saa moja jioni,na umpe mama,baba,mtu mkubwa yoyote akague .Usipofanya hivyo mara nyingi adhabu ilikua kufanya maswali mengine kumi kama hayo au anamwambia mwalimu wako akushugulikie shuleni.
4.Kwenda kanisani ni lazima,hili halikua na mjadala na hakukua na namna ya kulikwepa.
5.Hakuna kuangalia Tv wala sinema kabla ya saa nane mchana.Asubuhi ni walkati wa kazi,mapumziko ni Baada ya Lunch.Adhabu ya kuvunja hili ilikua ni kupewa kazi za kufanya,kwani kukaa unaangalia Tv maana yake huna kazi.Unaambiwa kashone vifungo vilivyotoka kwenye nguo zako,au kafute na kubrashi viatu vyako.
- Hizi ni baadhi ya ratiba na sharia au kanuni zilizonilea,na kunifanya niwe hivi nilivyo leo.ratiba hizi zilihusisha watoto wote,wakiume na wakike.Kwa ratiba kama hizi mtoto anajifunza kila kitu na anajifunza kujitegemea kwa kila kitu.
Ifike mahala muone aibu na mjiulize watoto wenu watakua kina baba au kina mama wanamna gani wakikua.Waswahili husema Samaki mkunje angali mbichi.Wewe unaengoja Samaki wako aive ndipo umkunje,utatia aibu na utaumbuka.
Pia ni vyema kujua kuwa,ni katika ufanyaji wa kazi hizi unaanza kuona na kutambua uwezo na vipaji vya watoto.Mpishi mzuri utaanza kumuona mapema,wale wanaopenda kusimamia wenzao ndio vipaji vya uongozi hivyo,kuna wale wa maneno mengi ila hawafanyi kazi nao utawajua na uanze kuwasaidia kubadili tabia hizo zisizofaa.
Hapa jikoni watoto wakija lazima niwape kazi yakufanya,kama hakuna kazi basi nampa kiti akae mlangoni(kukwepa ajali) tuongee mawili matatu wakati napika.Kwani najua anapoangalia niachofanya kula jambo anajifunza,na mara nyingi wanakua na maswali mengi juuu ya lile ninalolifanya.
Yangu ni haya tu kwa leo,yaliyobaki kazi kwako.Ukiamua kulea watoto kama mayai basi endelea ukijua unamuharibia mtoto maisha.
kwa mambo ya mapishi na malezi ingia hapa;http://tollyzkitchen.wordpress.com/
1 comment:
Nimeipenda sana sana hio.
Post a Comment