Showing posts with label Mtoto Atupwa. Show all posts
Showing posts with label Mtoto Atupwa. Show all posts

Thursday, 28 February 2013

Mtoto Mchanga aokotwa Kimara Baruti!!!!!!


Wasamariawema wakimsafisha uchafu mtoto mchanga baada ya kumuokota  katika eneo la bondeni huko Kimara Baruti Bondeni karibu na maeneo ya Ubungo Kibangu.
Kitoto hicho baada ya kusafishwa na wasamaria wema 
Leo asubuhi wasamaria wema  wamekiokota kitoto kichanga cha kiume huko Kimara baruti  bondeni karibu na Ubungo kibangu , wasamaria hao baada ya kumsafisha uchafu na damu waliamua kumpeleka mtoto huyo kwenye hospital ya Palestina kwa huduma ya kwanza na baadae  Hospital ya Mwananyamala ambako kuna kitengo maalumu cha kuhudumia watoto wachanga . Baadhi ya watu walioshuhudia tukio hilo wamesema kuwa kuna uwezekano wa mtoto huyo kutupwa leo asubuhi na hii imetokana na mtoto huyo  kukutwa akiwa hai na uwepo wa damu mbichi mwilini mwake .


Shukrani;Chinga One Blog

Tuesday, 19 February 2013

MTOTO MCHANGA AOKOTWA HUKO CHANIKA!!!!


Mtoto Mchanga Anayekadiriwa Kuwa na Mwezi Mmoja Amekutwa Ametupwa Na Mama Ambae Hadi sasa Hajafahamika.Mnamo tarehe 10-02-2013-saa kumi na Mbili jioni Eneo la Chanika Mtoto Huyo Aliokotwa Na Mohamedi Ramadhani Ambaye ni Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa na Kumpeleka Kituo Kidogo Cha Polisi Chanika.Ndipo Askari Wa Doria Ikawalazimu kumpeleka Mtoto huyo Hospitali ya Taifa ya Muhimbli Dar es Salam Kwahuduma Zaidi.

PICHA NA KHAMISI MUSSA)

Shukrani;KapingaZ Blog.