Wasamariawema wakimsafisha uchafu mtoto mchanga baada ya kumuokota katika eneo la bondeni huko Kimara Baruti Bondeni karibu na maeneo ya Ubungo Kibangu.
Kitoto hicho baada ya kusafishwa na wasamaria wema
Leo asubuhi wasamaria wema wamekiokota kitoto kichanga cha kiume huko Kimara baruti bondeni karibu na Ubungo kibangu , wasamaria hao baada ya kumsafisha uchafu na damu waliamua kumpeleka mtoto huyo kwenye hospital ya Palestina kwa huduma ya kwanza na baadae Hospital ya Mwananyamala ambako kuna kitengo maalumu cha kuhudumia watoto wachanga . Baadhi ya watu walioshuhudia tukio hilo wamesema kuwa kuna uwezekano wa mtoto huyo kutupwa leo asubuhi na hii imetokana na mtoto huyo kukutwa akiwa hai na uwepo wa damu mbichi mwilini mwake .
Shukrani;Chinga One Blog
No comments:
Post a Comment