Showing posts with label Watoto na Unyanyasaji. Show all posts
Showing posts with label Watoto na Unyanyasaji. Show all posts

Wednesday, 27 November 2013

Ukatili Kwa Watoto;Mtoto wa Miaka 5 Acharangwa Mapanga.


Mtoto mwenye umri wa miaka mitano, Benson Nilah (pichani), amejeruhiwa vibaya kwa kucharangwa mapanga akituhumiwa kuchuma mapera bustanini kwa mtu katika kijiji cha Madizini Manispaa ya Songea, mkoani Ruvuma. Mtoto huyo alijeruhiwa vibaya sehemu za usoni na mdomoni na kusababishwa ashonwe nyuzi sita, alipatwa na mkasa huo mwishoni mwa wiki iliyopita na anayetuhumiwa kufanya kitendo hicho ni Ronginus Haule (58), mkazi wa eneo hilo.
kusoma zaidi »http://www.chingaone.com/

Monday, 1 July 2013

Wanafunzi Watatu Wabakwa Na 'Mwalimu Bandia' Kiambu!!!!



Polisi katika eneo la Tigoni wanafanya uchunguzi kuhusiana na kisa ambapo wasichana watatu wa shule ya upili walibakwa. Ni kisa ambacho kimewaacha wengi midomo wazi kwa kuwa mshukiwa huyo alikuwa amepewa kandarasi ya kuwapa mafunzo ya nyimbo za kitamaduni wanafunzi hao miongoni mwa wengine kwa maandalizi ya mashindano ya 
kitaifa.

Habari kutoka;kenyacitizentv

Thursday, 28 March 2013

Ukatili/Unyanyasaji kwa watoto wetu!!




Hivi ndivyo  alivyochomwa  chomwa  mwilini na kitu chenye ncha kali
 Na Raymond  Francis, Iringa  
Vituko mjini Iringa haviwezi kuisha kama jamii haitakubali kwa moyo mmoja kupambana na ukatili wa kijinsia.
Huyu ni Binti ZAWAD KARIM  miaka 16 mkazi wa mshindo nyuma ya banki ya NBC manispaa ya Iringa amepigwa na hatimaye kunyweshwa mkojo na mama yake mdogo aitwaye Ever ubamba.

Tukio lilikuwa hivi:

Zawadi ambaye kimsingi anaishi na mama yake mzazi ambaye kwa kipindi hicho dada mtu huyo alikuwa anaumwa. Ever alikuwa nje na marafiki zake ndipo mama yake mdogo huyo akamwiita ndani ya nyumba yao hiyo wanayoishi mtaa wa mshindo
                      

Baada ya kumwita na kisha mtoto huyo kushindwa kusikia baadaye aliitika na kuingia ndani ndipo alipo ambiwa avue nguo zote amri iliyotolewa na mama yake huyo mdodo Ever baada ya muda mfupi Zawadi alianza kupokea kipigo kikali kutoka kwa mama yake huyo mdogo.

Katika kipigo hicho Zawadi inadaiwa kwamba alipigwa pamoja na kunyweshwa mkojo kutoka kwa mama yake mdogo huyo.

Zawadi ambaye ni mtoto wa kuzaliwa na Dada yake Ever inadaiwa kipigo hicho kimesababishwa na tuhuma kwamba eti familia hiyo haina mtoto kama yeye zawadi.

Zawadi inadaiwa aliwahi kwenda zanzibar kwa nia ya kufanya kazi na baada ya muda mama yake mzazi ambaye jina lake bado halijafahamika alimpigia simu arudi nyumbani na mara baada ya kurudi ndipo kutokuelewana huko kukajitokeza.

Aidha taarifa za ndani kuhusu tukio hilo zinasema kuwa Mmama yake Msichana Zawadi alitupwa akiwa mchanga na kuokotwa na wasamalia wema na hatimaye kulelewa na Bibi yake ambaye hata hivyo amefariki duni.
Kisa cha yote hayo ni madai ya mtoto zawadi kuomba aneshwe Baba yake mzazi ili walau aweze kupata pumziko la adha anazo zipata kutoka kwa ushirika wa ndugu zake hao.

Zawadi pamoja na majirani wameuambia mtandao huu kuwa vitu vilivyo tumika kumwadhibu vilikuwa ni pamoja na nyaya za simu,mkandaa,na vipande vya chupa katika kumchoma navyo.

Hata hivyo hadi mtandao huu unachapisha taarifa hii watuhumiwa wa tukio hili yaani Mama mzazi pamoja na Mama mdogo wa Zawadi wanashikiliwa na jeshi la polisi kitengo cha dawati la jinsia kwa mahojiano zaidi.


shukrani;http://francisgodwin.blogspot.co.uk/

Tuesday, 19 February 2013

Mama aliyemlisha Kinyesi na kumchoma moto mtoto ahukumiwa kifungo cha maisha jela!!!!!!

Wilvina Mkandala (24) akitolewa mahakamani mara tu baada ya kusomewa hukumu ya kifungo cha maisaha 
 Mtoto Aneth kabla ya kukatwa kwa mkono wake wa kushoto


Mtoto Aneth mara baada ya kukatwa mkono wa kushoto kwa ujumla mtoto huyu anaendelea vizuri na alishatoka hospitalini.



Na Ezekiel Kamanga, Mbeya.
WILIVINA MKANDALA mwenye umri wa miaka 24 ameukumiwa kutumikia kifungo cha maisha jela baada ya kukutwa na hatia ya kumlisha mtoto ANETH GASTO mwenye umri wa 5 mitano kinyesi na na kumuunguza kwa maji ya moto

Akisoma hati ya mashtaka mwendesha mashtaka wa serikali ACHIREY MULISA ameiomba mahakama hiyo kutoa adhabu kali kwa mshtakiwa ili iwe fundisho kwa watu wegine wenye tabia kama hiyo

Akisoma hukumu hiyo kwa muda wa dakika hamsini hakimu mfawidhi wa mahakama ya wilaya mbeya GILBERT NDEURUO ameridhishwa na   na ushahidi uliotolewa na upande  wa Jamuhuri kwamba  mshtakiwa amtenda kosa kinyume cha sheria  cha makosa ya jinai namba 222(a)sura  ya kumi na sita ya marekebisho ya mwaka 2002

Hata hivyo ameiomba serikali kutunga sheria ya kumlinda  mtoto kutokana na vitendo vilivyokithiri kwa  watoto ambapo amesema tanzania haina sheria ya kulinda mtoto

Akijitetea mahakamani mtuhumiwa huyo   ameiomba mahakama kumpunguzia adhabu kwani anategemewa na familia sababu ambazo zilipingwa na mahakama hiyo.

Monday, 18 February 2013

Case File: - "She killed when she was 10"



Wazazi/Walezi tujifunze kuishi Vyema na dada/walezi wanaotusadia kazi za nyumbani.
Umejifunza nini kupitia dada huyu?