Wilvina Mkandala (24) akitolewa mahakamani mara tu baada ya kusomewa hukumu ya kifungo cha maisaha |
Mtoto Aneth mara baada ya kukatwa mkono wa kushoto kwa ujumla mtoto huyu anaendelea vizuri na alishatoka hospitalini. |
Na Ezekiel Kamanga, Mbeya.
WILIVINA MKANDALA mwenye umri wa miaka 24 ameukumiwa kutumikia kifungo cha maisha jela baada ya kukutwa na hatia ya kumlisha mtoto ANETH GASTO mwenye umri wa 5 mitano kinyesi na na kumuunguza kwa maji ya moto
Akisoma hati ya mashtaka mwendesha mashtaka wa serikali ACHIREY MULISA ameiomba mahakama hiyo kutoa adhabu kali kwa mshtakiwa ili iwe fundisho kwa watu wegine wenye tabia kama hiyo
Akisoma hukumu hiyo kwa muda wa dakika hamsini hakimu mfawidhi wa mahakama ya wilaya mbeya GILBERT NDEURUO ameridhishwa na na ushahidi uliotolewa na upande wa Jamuhuri kwamba mshtakiwa amtenda kosa kinyume cha sheria cha makosa ya jinai namba 222(a)sura ya kumi na sita ya marekebisho ya mwaka 2002
Hata hivyo ameiomba serikali kutunga sheria ya kumlinda mtoto kutokana na vitendo vilivyokithiri kwa watoto ambapo amesema tanzania haina sheria ya kulinda mtoto
Akijitetea mahakamani mtuhumiwa huyo ameiomba mahakama kumpunguzia adhabu kwani anategemewa na familia sababu ambazo zilipingwa na mahakama hiyo.
KwaHabari zaidi;http://chimbukoletu.blogspot.co.uk/
2 comments:
Naombeni mnipatie namba ya mlezi wa huyu mtoto japo na mimi nikampatie chochote kwa ajili ya malezi yake. Imeniuma sana. Namba zangu ni 0767 233281
Asante sana mdau.ngoja nikutafutie..
Ubarikiwe sana.
Post a Comment