Friday 26 July 2013

Watoto Wetu;Hadithi za Leo;Kisima cha Kwanza na Filimbi ya Kasa!!!!!!!!!!




Watoto,Wazazi/Walezi.Nimatumaini yangu wote hamjambo na Mnaendelea Vyema na Likizo kwa Watoto Mnaoishi Nga'mbo,Watoto wa Nyumbani/Afrika nanyi manaendelea vyama na Masomo.

Mmependa Hadithi za Leo?
Jee mmejifunza nini?
Nawatakia Mapumziko mema ya mwisho wa wiki na Muwe watoto Wema kwa Wazazi/Walezi na Jamii Pia.

Shukrani;bookboxinc

Ni mimi ;shangazi/Mama yenu,Rachel siwa[Kachiki]

Monday 22 July 2013

Watoto na Sherehe;Miaka 15 ya Da'Sandra-Neema!!!!






Natumai wote wazima wa Afya.. Watoto  Wa Nga'mbo mnaendelea vyema na Likizo. mlio Afrika  mnaendelea vyema na masomo.

Leo tuangalie  sherehe ndogo ya Da'Sandra-Neema ametimiza miaka 15.Ilikuwa sherehe ndogo ya kifamilia.



Sherehe hii ndogo iliandaliwa/simamiwa na da'Tracey-Sarah..kuanzia mapambo na vitu vyote.

Familia ya Isaac inawatakia Watoto wote waliozaliwa Mwezi huu na wengine wote Maisha mema yenye Amani,Upendo,Baraka na Furaha.
  
 Kama unapicha/Matukio na mengineyo,usisite kutumia kupia Email;rasca@hotmail.co.uk.

Wote Mnakaribishwa.


Thursday 18 July 2013

Saturday 6 July 2013

Watoto Wetu,Katuni ya Leo-Kiriku na Mchawi sehemu ya 1-4 kwa kiswahili!!


Leo Jua limewaka ni kucheza tuu!!!!








Ni Matumaini yangu watoto wote hamjambo na mnaendelea vyema...mlio nyumbani Tanzania mnamalizia Likizo..wa huku Nga'mbo  hapa Uk...Mnakaribia kuanza Likizo..hapa tulipo COVENTRY Leo Jua linawaka vizuri kabisa,Watoto watapata muda mzuri wa kucheza na kufurahi .

Haya Leo Tujifunze kupitia katuni zilizo Tafsiliwa kwa Lugha ya Kiswahili..leo tunaye KIRIKU!!!

Usikose kutoa maoni yako..kama wewe hujui Kiswahili ni muda mzuri wa kujifunza kupitia katuni hizi..mwambie Mama/Baba,Walezi au mtoto/mtu anayejua Kiswahili akusaidie...

Kama una lolote kuhusu Watoto,Wazazi/Walezi,Usisite kututumia kupitia Email;rasca@hotmail.co.uk.

Asanteni sana na Karibuni Wote.

Monday 1 July 2013

Wanafunzi Watatu Wabakwa Na 'Mwalimu Bandia' Kiambu!!!!



Polisi katika eneo la Tigoni wanafanya uchunguzi kuhusiana na kisa ambapo wasichana watatu wa shule ya upili walibakwa. Ni kisa ambacho kimewaacha wengi midomo wazi kwa kuwa mshukiwa huyo alikuwa amepewa kandarasi ya kuwapa mafunzo ya nyimbo za kitamaduni wanafunzi hao miongoni mwa wengine kwa maandalizi ya mashindano ya 
kitaifa.

Habari kutoka;kenyacitizentv