Tuesday 25 February 2014

Watoto Na Malezi; Mapenzi ya Watoto!!!!


Watoto wanamambo yao...Kuna wakati  Wanacheza,Kuna Wakati Wanagombana,Kuna Wakati wanaoneana Huruma,Kuna Wakati Lao Moja,Kuna Wakati kila mmoja anataka Lake,Maamuzi,Yeye Zaidi.

Pia Kuna wakati Mkubwa anataka kuonyesha ukubwa wake,Kuna Wakati mdogo anaanza uchokozi na kutaka kuonewa Huruma tuu kwasababu ya udogo wake.

Wazazi/Walezi.. Na Kauli Zao;Muachie mtoto,Wewe nawe Mkubwa Mzima,Unaona ukosawa naye..huyu ni mdogo wako...Na Mengine Meeengi.
Kama una la Zaidi Ongezeaa......

Jee ni Kweli  Watoto waliofuatana Huwa hawapendani,Hugombana sana?



Saturday 22 February 2014

Watoto wetu;movie ya leo-Ella Enchanted Full Movie!!!!!!




Natumaini Watoto,Wazazi/Walezi wote Mnaendelea Vyema.
Mliokuwa kwenye Likizo mjiandae vyema kurudi Shule.

Jee nini mmejifunza kupitia Video/sinema hii?

Nawatakia kila la Kheri.

Wenu Shangazi/Mama yenu Rachel.

Friday 14 February 2014

Da'Nadia Nyembo Fundikira Atimiza Miaka 4!!!!


Tunakutakia Afya njema Maisha marefu katika  kumbukumbu ya Siku yak ya kuzaliwa na Siku Zote Maishani mwako, Mwanetu kipenzi NADIA NYEMBO FUNDIKIRA .
MWENYEEZI MUNGU akujahalie upendo kwa watu wote .
Daddy,Mom n Naomi  we  L.V.U
HAPPY BIRTHDAY NADIA......Mwaaaahhh. 


Watoto Na Jamii;Tunakutakila,Kila la Heri,Baraka,Furaha,Amani na Upendo.MUNGU azidi kukubariki na kukulinda siku zote.

Wednesday 12 February 2014

Da'Naomi Nyembo Fundikira Atimiza Miaka 6!!!!!!


A.aleykum ndugu zangu wapendwa,Tuna kila sababu ya kumshukuru mwenyezi MUNGU subhukhanna watakhara kwa kuweza kutupa pumzi mpaka leo hii Tukishuhudia kumbukumbu ya kuzaliwa kwa mwanetu Naomi Nyembo Fundikira kutimiza miaka 6 : HAPPY BIRTHDAY MY LOVELY DAUGHTER NAOMI.DADDY,MOM N NADIA LOVES U.


Watoto Na Jamii;
Nasi tunamtakia kila lililojema  Maishani,MUNGU azidi kuwalinda kila iitwapo Leo.

Kama unalolote unapenda kushirikiana nasi,Tuma kupitia Email;rasca@hotmail.co.uk.

Monday 10 February 2014

[AUDIO]: Kipindi cha familia kutoka Jamii Productuion...BAJETI KATIKA FAMILIA‏


Bwn Solomon, Sunday Shomari na Herriet Shangirai wakijadili jambo ndani ya studio za Jamii Production. Washington DC
Karibu katika kipindi cha FAMILIA kutoka Jamii Production.
Katika kipindi hiki, tumejadili suala la BAJETI KATIKA FAMILIA.
umuhimu wake, namna ya kulitekeleza na mengine mengi.
Wachangiaji studio walikuwa ni Herriet Shangirai, Sunday Shomari, Solomon na Mubelwa Bandio
KARIBU UUNGANE NASI