Tuesday 19 February 2013

Mama aliyemlisha Kinyesi na kumchoma moto mtoto ahukumiwa kifungo cha maisha jela!!!!!!

Wilvina Mkandala (24) akitolewa mahakamani mara tu baada ya kusomewa hukumu ya kifungo cha maisaha 
 Mtoto Aneth kabla ya kukatwa kwa mkono wake wa kushoto


Mtoto Aneth mara baada ya kukatwa mkono wa kushoto kwa ujumla mtoto huyu anaendelea vizuri na alishatoka hospitalini.



Na Ezekiel Kamanga, Mbeya.
WILIVINA MKANDALA mwenye umri wa miaka 24 ameukumiwa kutumikia kifungo cha maisha jela baada ya kukutwa na hatia ya kumlisha mtoto ANETH GASTO mwenye umri wa 5 mitano kinyesi na na kumuunguza kwa maji ya moto

Akisoma hati ya mashtaka mwendesha mashtaka wa serikali ACHIREY MULISA ameiomba mahakama hiyo kutoa adhabu kali kwa mshtakiwa ili iwe fundisho kwa watu wegine wenye tabia kama hiyo

Akisoma hukumu hiyo kwa muda wa dakika hamsini hakimu mfawidhi wa mahakama ya wilaya mbeya GILBERT NDEURUO ameridhishwa na   na ushahidi uliotolewa na upande  wa Jamuhuri kwamba  mshtakiwa amtenda kosa kinyume cha sheria  cha makosa ya jinai namba 222(a)sura  ya kumi na sita ya marekebisho ya mwaka 2002

Hata hivyo ameiomba serikali kutunga sheria ya kumlinda  mtoto kutokana na vitendo vilivyokithiri kwa  watoto ambapo amesema tanzania haina sheria ya kulinda mtoto

Akijitetea mahakamani mtuhumiwa huyo   ameiomba mahakama kumpunguzia adhabu kwani anategemewa na familia sababu ambazo zilipingwa na mahakama hiyo.

2 comments:

Anonymous said...

Naombeni mnipatie namba ya mlezi wa huyu mtoto japo na mimi nikampatie chochote kwa ajili ya malezi yake. Imeniuma sana. Namba zangu ni 0767 233281

Rachel Siwa said...

Asante sana mdau.ngoja nikutafutie..
Ubarikiwe sana.